Posts

Showing posts from August 2, 2023

WAKAZI WA DODOMA WASHAURIWA KUPIMA UDONGO KABLA YA KILIMO

Image
Na. Dennis Gondwe, NZUGUNI WAKAZI wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wametakiwa kujenga utamaduni wa kupima afya ya udongo ili kujua mahitaji ya virutubishi kwa udongo vitakavyosaidia kupata mazao mengi na bora. Mkuu wa Divisheni ya Kilimo Mjini, Yustina Munishi Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Divisheni ya Kilimo mjini katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Yustina Munishi alipokuwa akiongelea umuhimu wa afya ya udongo kwa mkulima katika kuzalisha mazao bora na yenye tija. Munishi alisema kuwa kujua afya ya udongo ni muhimu sana kwa mkulima. “Napenda kuwataarifu kuwa kujua afya ya udongo ni muhimu sana kwa mkulima kabla ya kuanza kilimo alichokusudia. Kujua afya ya udongo kunamuwezesha mkulima kujua kiasi cha nyongo au tindikali kilichopo katika udongo. Ukijua afya ya udongo utajua ni zao gani uzalishe na linahitaji virutubisho gani na uweke mbolea ya aina gani na kwa kiasi gani ili uweze kupata mazao yaliyo bora. Hii ni muhimu kwa sababu watu wengi wanadanganyika kwa kuona udongo m...