Posts

Showing posts from September 24, 2023

KATA YA CHAMWINO YATAKIWA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI MKATABA WA LISHE

Image
  Na. Dennis Gondwe, CHAMWINO KATA ya Chamwino imetakiwa kusimamia utekelezaji wa mkataba wa Lishe kwa mujibu wa maelekezo ya serikali ili kukabiliana na tatizo la utapiamlo katika jamii. Kauli hiyo ilitolewa na Diwani wa Kata ya Chamwino, Jumanne Ngede aliyekuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe Mtaa wa Mailimbili aliyofanyika katika mtaa wa Mailimbili. Ngede alisema kuwa ni jambo zuri kwa wataalam na Afisa Mtendaji wa Kata ya Chamwino kusimamia suala la Lishe kutokana na umuhimu wake katika jamii. Alisema kuwa kutokana na umuhimu wake, serikali ilisaini mkataba wa Lishe na makundi mbalimbali ili watekeleze mkataba huo kwa kuhakikisha elimu ya Lishe inatolewa na utekelezaji wa mkataba huo. Kwa upande wake Afisa Mtendaji Kata ya Chamwino, Lucas Nkelege alisema kuwa suala la utekelezaji wa mkataba wa Lishe ni maelekezo ya serikali yanayotakiwa kutekelezwa kwa uzito mkubwa. “Tumeshasaini mkataba wa Lishe, utakumbuka Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Has...