Posts

Showing posts from November 22, 2025

Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wameshiriki kongamano la Maafisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Dodoma kwa siku mbili likiwa na lengo la kukumbushana majukumu ya kazi, kupitia sera mpya zilizoandaliwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum na kutoka na mpango kazi mpya wa kutekeleza katika maeneo yao ya kazi.

Image
  Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wameshiriki kongamano la Maafisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Dodoma kwa siku mbili likiwa na lengo la kukumbushana majukumu ya kazi, kupitia sera mpya zilizoandaliwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum na kutoka na mpango kazi mpya wa kutekeleza katika maeneo yao ya kazi.

Maafisa Mazingira Kanda Namba Sita waanza ziara ya kutoa elimu ya usafi wa mazingira sambamba na uhamasishaji wananchi kuchangia ada ya uzoaji taka.

Image
  Maafisa Mazingira Kanda Namba Sita waanza ziara ya kutoa elimu ya usafi wa mazingira sambamba na uhamasishaji wananchi kuchangia ada ya uzoaji taka. ‎ ‎Watumishi Kanda Namba Sita waanza mkakati wa kuhakikisha kata zinazounda kanda hiyo usafi wa mazingira unaimarika. ‎ ‎Akizungumza katika kikao kilichofanyika baina ya watumishi wa Kanda na viongozi wa Mtaa wa Mbwanga, Afisa Afya Kanda Namba Sita, Zainab Iddi alisema kuwa kuishi kwenye mazingira safi ni haki na wajibu wa kila mwananchi ‎ ‎Alisema kuwa usafi wa mazingira husaidia afya kuwa imara na salama. "Mtaa wa Mbwanga ni mojawapo wa mitaa ambayo tunataka wananchi waimarike katika suala la usafi wa mazingira. Katika suala la kiafya hairuhusiwi kutunza taka kwa mda mrefu au kuzichoma kwasababu kuna baadhi ya kemikali zinaweza kuleta madhara kwa binadamu" alisema Iddi ‎ ‎Aidha aliongeza kuwa wananchi wanatakiwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa na Serikali. ‎ ‎Akisoma sheria za usafi wa mazingira Afisa Mazingir...

Maafisa kutoka Kanda Namba Nne wakípima bango kwaajili ya kutathmini kodi ya bango kwa mujibu Sheria ndogo ya Ada na Ushuru wa Mabango na Matangazo ya Mwaka 2017.

Image
  Maafisa kutoka Kanda Namba Nne wakípima bango kwaajili ya kutathmini kodi ya bango kwa mujibu Sheria ndogo ya Ada na Ushuru wa Mabango na Matangazo ya Mwaka 2017. Sambamba na hilo wanaendelea kutoa elimu ya ulipaji kodi kwa wananchi wanaowatembelea ili kuhakikisha halmashauri inakusanya mapato stahiki

Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma imefanya ziara katika Kanda Namba Tatu ya kukagua miradi ya maendeleo.

Image
  Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma imefanya ziara katika Kanda Namba Tatu ya kukagua miradi ya maendeleo. Miradi iliyotembelewa ni Shule ya Msingi Mahungu na Kituo cha Afya Kizota.

Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma imefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo Kanda Namba Mbili ambapo wakati wa ukaguzi walisisitiza ubora, thamani ya fedha na kasi ya utekelezaji kwa manufaa ya wananchi.

Image
  Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma imefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo Kanda Namba Mbili ambapo wakati wa ukaguzi walisisitiza ubora, thamani ya fedha na kasi ya utekelezaji kwa manufaa ya wananchi.

Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma imefanya ziara katika Kanda Namba Moja kukagua miradi ya maendeleo. Mradi uliotembelewa ni Shule ya Msingi Kaloleni wenye thamani ya shilingi 151,000,000 ambapo mradi huo upo katika utekelezaji

Image
  Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma imefanya ziara katika Kanda Namba Moja kukagua miradi ya maendeleo. Mradi uliotembelewa ni Shule ya Msingi Kaloleni wenye thamani ya shilingi 151,000,000 ambapo mradi huo upo katika utekelezaji

Maafisa kutoka Kanda Namba Nne wamefanya ziara katika Migahawa mikubwa kwa lengo la kukagua Leseni za Biashara na pia ulipaji wa Kodi ya Huduma yaani Service Levy huku wakiendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa kulipa kodi kwa wakati

Image
  Maafisa kutoka Kanda Namba Nne wamefanya ziara katika Migahawa mikubwa kwa lengo la kukagua Leseni za Biashara na pia ulipaji wa Kodi ya Huduma yaani Service Levy huku wakiendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa kulipa kodi kwa wakati

"Lakini kwenye uwezeshaji Wananchi kiuchumi tunapoliangalia kundi la Maendeleo ya Jamii,tunaona kuwa ni watu ambao wanatakiwa kuona mabadiliko ya kijamii kwa ujumla ya kiuchumi yanatokea kutokana na kazi zao".

Image
  "Lakini kwenye uwezeshaji Wananchi kiuchumi tunapoliangalia kundi la Maendeleo ya Jamii,tunaona kuwa ni watu ambao wanatakiwa kuona mabadiliko ya kijamii kwa ujumla ya kiuchumi yanatokea kutokana na kazi zao". Ni maneno ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule wakati akifungua kikao kazi cha siku 2 cha Maafisa Maendeleo ya jamii kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Dodoma.

Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma imefanya ziara katika kanda Namba Tatu ya kukagua miradi ya maendeleo.

Image
  Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma imefanya ziara katika kanda Namba Tatu ya kukagua miradi ya maendeleo. Miradi iliyotembelewa ni Hospitali ya Jiji la Dodoma yenye ujenzi wa Jengo la Upasuaji wenye thamani ya shilingi 337,889,130 zilizoingizwa tarehe 30 Agosti, 2025. Mradi huo umefikia asilimia 38. Mradi mwingine uliotembelewa ni pamoja na Jengo la Wodi ya Wanawake lenye thamani ya shilingi 252,426,200 na ujenzi wa jengo la kufulia lenye thamani ya shilingi 209,684,670.

Maadhimisho ya Wiki ya Lishe kupitia Dodoma FM jijini DOdoma

Image
  Maafisa Lishe Jiji la Dodoma wamefanya shughuli mbalimbali katika Wiki ya Lishe ikiwemo utoaji wa elimu ya lishe kupitia vyombo vya habari na kwa kutembelea vituo vya kulelea watoto kwaajili ya kupima afya. ‎ ‎Maadhimisho ya Siku ya Lishe Kitaifa ambayo yalianza tarehe 17 Novemba 2025 yanatarajiwa kuhitimishwa leo tarehe 21 Novemba, 2025. ‎ ‎Akizungumza katika kipindi cha Dodoma Live kinachorushwa na Kituo cha Redio Dodoma Fm, Afisa Lishe Kituo cha Afya Makole, Frida Mollel alisema kuwa kila mmoja anatakiwa kuzingatia makundi sita ya chakula. "Katika maisha ya kawaida ya binadamu makundi sita ya chakula yanapatikana kiurahisi mfano mboga za majani, matunda, dagaa hata mafuta ya kupikia. Jambo la kuzingatia ni kwamba kuna baadhi ya vyakula havitakiwa kuliwa kwa pamoja kwasababu vinafanya kazi moja" alisema. ‎ ‎Mollel alisisitiza kwa mifano juu ya aina ya vyakula vinavyopaswa kuepukwa kuliwa kwa pamoja na vyenye kazi moja kwenye mwili wa binadanu. "Mfano viazi, ndiz...

Sungura kitoweo cha gharama nafuu

Image
‎Na. Mwandishi Wetu, HOMBOLO MAKULU ‎ ‎Maadhimisho ya Wiki ya Lishe katika Jiji la Dodoma yafanyika kupitia zoezi la ugawaji wa Sungura kwa kaya zenye kipato cha chini kwa lengo la kuzisaidia kupata makundi yote ya chakula bila kuathiriwa na kipato kidogo walichonacho. ‎ ‎Maadhimisho hayo yalianza tarehe 17 Novemba, 2025 na yanatarajiwa kuhitimishwa leo tarehe 21 Novemba, 2025. ‎ ‎Akizungumza na waandishi wa habari katika zoezi hilo lililofanyika Kata ya Hombolo Makulu, Daktari wa Mifugo kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dr. Innocent Kimweri alisema kuwa ufugaji wa Sungura hauna gharama ya kuwatunza na ni kitoweo kizuri kwaajili ya lishe bora. ‎ ‎Aliongeza kuwa, suala la lishe wanalihamasisha katika kaya zenye kipato cha chini ili kuwapa elimu ya kutosha kufahamu makundi muhimu ya chakula. "Suala la lishe ni mtambuka, pamoja na kwamba sisi ni maafisa mifugo, tunazingatia ulaji wa mlo kamili. Sungura ni rahisi kutunza kwasababu wanakula tu majani, mabaki ya vyakula na h...

Jiji la Dodoma laendesha kampeni ya elimu kwa wakulima

Image
  Halmashauri ya Jiji la Dodoma inaendelea na kampeni ya kutoa elimu kwa wakulima katika kuelekea msimu wa kilimo kwa mwaka 2025/2026 ambapo wakulima wameelekezwa kulima mazao yanayostahimili mvua kidogo kama vile mtama, uwele na mihogo. Akizungumza na wananchi waliojitokeza kupata elimu hiyo katika Kata ya Chihanga, Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Agnes Woisso alisema kuwa wananchi wanapaswa kuzingatia ushauri wa kitaalam wanaopewa ili wavune mazao mengi. Alishauri kuwa wakulima wote wanapaswa kuachana na kilimo cha mazoea kwasababu kinawarudisha nyuma na kuwakosesha mavuno yenye tija. Alisema kuwa kwa mujibu wa utabiri wa hali ya hewa mvua zitakuwa za wastani na chini ya wastani ambapo zitaanza kunyesha wiki mbili za kwanza za mwezi Disemba na zitaisha wiki ya tatu na nne za mwezi Aprili.

Jiji la Dodoma laendesha zoezi la Upimaji Afya na Lishe Tehillah Daycare Centre

Image
  Mtaalamu wa Lishe kutoka Kituo cha Afya Makole, Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Frida Mollel ametembelea kituo cha kulelea watoto chini ya miaka mitano cha Tehillah Daycare Centre na kufanya vipimo vya hali ya Afya na Lishe kwa watoto hao ili kubaini maendeleo ya lishe na kutoa ushauri stahiki kwa walezi.