Posts

Showing posts from January 13, 2025

Elimu ni haki ya watoto wenye mahitaji maalum Kata ya Ipagala

Image
Na. Coletha Charles, IPAGALA Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeendelea na jitihada ya utambuzi wa watoto wenye mahitaji maalum kiafya kwa lengo la kujiunga na elimu ya awali na msingi kwa mwaka wa masomo 2025 katika Kata ya Ipagala. Akizungumza wakati zoezi hilo, Afisa Elimu wa Kata ya Ipagala, Veronica Mpanda, aliwaomba wazazi kuwapeleka watoto wenye mahitaji maalum shule kwa sababu wanahaki ya kupata elimu kama watoto wengine kulingana na sera ya elimu jumuishi kwa kuwa miundombinu imara ipo kwa ajili yao. Alisema kuwa zoezi hilo linalenga kutambua idadi na aina ya mahitaji ya watoto hao ili kuweka mipango madhubuti ya kuwahudumia. “Zoezi hili la uandikishaji lilitakiwa lifanyike katika Shule ya Msingi ya Ipagala B, lakini hatujafanikiwa kupata mtoto hata mmoja mwenye mahitaji maalum japo zoezi hili ni endelevu na tunatambua kwamba elimu ni haki ya kila mtoto na kupitia zoezi hili tutahakikisha kuwa hakuna mtoto anayebaki nyuma kwa sababu ya changamoto yoyote” alisema Mpanda. ...