WAZAZI MTAA WA MAZENGO WASHAURIWA KULEA WATOTO KATIKA MAADILI
Na. Dennis Gondwe, CHANG’OMBE WAZAZI wa Mtaa wa Mazengo Kata ya Chang’ombe wametakiwa kijikita katika malezi ya watoto ili wawe na maadili mema yatakayowawezesha kuwa raia wema na wawajibikaji katika jamii. Afisa Ustawi wa Jamii wa Kata ya Chang’ombe, Debora Kanuya Kauli hiyoilitolewa na Afisa Ustawi wa Jamii wa Kata ya Chang’ombe, Debora Kanuya alipokuwa akiongea na wananchi wa Mtaa Mazengo kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kufanyika katika Ofisi ya CCM Tawi la Chang’ombe Magharibi jijini Dodoma. Kanuya alisema “ninawaomba sana akina mama wa Mtaa wa Mazengo, tuwe na maneno mazuri kwa watoto wetu ili watoto wanapokuwa wawe wanafahamu maneno mazuri, wasiwe na maneno ya matusi na maneno ya mtaani. Lakini pia kuna baadhi ya akina mama ambao wamekuwa wakipiga sana watoto wao na kutoa lugha ya matusi. Unakuta baadhi ya kina mama wametelekezwa kwa hiyo zile hasira za kutelekezwa wanazihamishia kwa watoto, huo ni ukatili. Niwaombe sana wanawake...