Posts

Showing posts from August 24, 2023

WAFANYABIASHARA SOKO LA SABASABA WAHAKIKISHIWA KUFANYABIASHARA HADI MWISHO MWAKA WA FEDHA 2023/2024

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma kimewahakikishia wafanyabiashara wa Soko la Sabasaba kuwa hawataondolewa katika soko hilo hadi Mwezi Julai mwakani ili waendelee kutekeleza majukumu yao bila wasiwasi. Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa katika mkutano wa hadhara na wafanyabiashara wa Soko la Sabasaba jijini Dodoma. Kimbisa alisema “napenda kuwafahamisha kuwa hadi mwezi Julai mwakani hakuna mfanyabiashara atakayebughudhiwa hadi halmashauri itakapopata fedha za kuendeleza soko hilo. Halmashauri wakipata fedha hizo lazima tukae pamoja na kukubaliana wanaanza na jambo gani na kuendelea na jambo gani. Tunafahamu jiji mtajenga kwa awamu, mtashirikiana na uongozi wa soko ili kuhakikisha huduma zinakuwa bora”. Akiongelea daladala kuingia katika Soko la Sabasaba, alisema kuwa soko hilo siyo stendi ya daladala. “Daladala zinapopaki kwa sasa si sawa. Daladala zilipo zitaua w...