Posts

Showing posts from September 18, 2026

Soko la Mnada mpya wapangwa wafanyabiashara 150

Image
Na. Mwandishi wetu, KIZOTA   Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeendelea kuboresha Soko la Mnada Mpya lililopo Kata ya Kizota, kwa kufanya ukarabati wa barabara na kuwapangia wafanyabiashara wadogo maeneo ya kufanyia biashara ndani ya soko hilo, hatua inayolenga kuweka mazingira bora na yenye utaratibu. Akizungumza kuhusu zoezi hilo, Afisa Biashara wa Kanda Namba Tatu, Halmashauri ya Jiji la Dodoma Stephen Maufi alisema kuwa halmashauri imewapangia wafanyabiashara maeneo kulingana na aina ya biashara zao, zikiwemo samaki, matunda na mbogamboga, mishikaki, kuku na viazi. Alisema kuwa zaidi ya wafanyabiashara 150 wamepangiwa maeneo ndani ya soko hilo.   Maufi alisema kuwa awali wafanyabiashara wapatao 55 walikuwa wakifanya biashara nje ya eneo la soko, hivyo zoezi hilo limefanyika kuwaingiza ndani ya soko na kuhakikisha shughuli za biashara zinafanyika katika maeneo yaliyotengwa.   Alisisitiza kuwa maeneo hayo yametolewa bure kwa ajili ya kufanyia biashara na si kw...