RAIS, DKT. SAMIA ATOA FIDIA YA BILIONI 4.5 KWA WAKAZI DODOMA
Na. Queen Peter, DODOMA WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amesema wananchi takribani 496 wa Jiji la Dodoma watapatiwa fidia ya kiasi cha Tsh. Bil. 4.5 ambazo tayari zimetolewa na Rais, Dkt. Rais, Dkt. Samia Suluhu ili kulipa wananchi waliotwaliwa maeneo yao kwa ajili ya uendelezaji wa Jiji hilo. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa (kushoto) akiongea na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde (kulia) katika Kliniki ya Ardhi jijini Dodoma Waziri Silaa alisema hayo wakati wa zoezi la utatuzi wa migogoro ya Ardhi linaloendelea katika uwanja wa Ofisi ya Ardhi Mkoa wa Dodoma alipofika hapo kwa lengo la kuongea na wananchi ikiwemo kukabidhi hati kwa baadhi ya wananchi. Waziri Silaa ameongeza kuwa wananchi watakao lipwa fidia hiyo ni wale ambao viwanja vyao vilitwaliwa kimakosa na kuzua malalamiko mengi hivyo hiyo ni hatua muhimu ya kutatua kero ya muda mrefu kwa wananchi hao. Aidha, aliwataka watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba...