AFISA MTENDAJI KATA YA CHAMWINO APEWA CHETI UTEKELEZAJI MKATABA WA LISHE JIJI LA DODOMA
Na. Dennis Gondwe, DODOMA AFISA Mtendaji wa Kata ya Chamwino, Lucas Nkelege amepongezwa na kupatiwa cheti kwa kufanya vizuri katika utekelezaji wa Mkataba wa Lishe katika jijini Dodoma. Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri akimkabidhi cheti kutambua kazi nzuri ya utekelezaji Mkataba wa Lishe Afisa Mtendaji Kata ya Chamwino, Lucas Nkelege Pongezi hizo zilitolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Lishe Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri alipoongoza Kikao cha Tathmini ya Mkataba wa Lishe kwa robo ya nne kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Shekimweri ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma alisema kuwa suala la lishe ni muhimu kwa wilaya yake na maafisa watendaji wa kata wana wajibu wa kusimamia lishe katika maeneo yao. “Ndugu zangu, napenda kuwaambia tunatakiwa kuwa na tafsiri pana na dhamira ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusiana na suala la lishe. Tuhakikishe watoto wanapata chakula shuleni. Wale wote amb...