Na. Asteria Frank, DODOMA Wananchi wameshauriwa kujitokeza kwa wingi kusikiliza elimu inayotolewa na wahamasishaji kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa njia mbalimbali ikiwemo kikundi maalum cha ngoma cha Dodoma Jiji Mtaa kwa Mtaa Uchaguzi Festival. Afisa Utamaduni wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Desdery Kuzenza akihamasisha mamia ya wananchi wa Swaswa Mnarani Hayo, yalisemwa na Afisa Utamaduni wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Desdery Kuzenza alipokuwa akihamasisha wananchi kujitokeza kutumia haki yao ya msingi na ya kikatiba ya kupiga kura na kuwachagua viongozi watakaowafaa kwa manufaa ya maendeleo ya mitaa yao. “Naomba nitoe rai kwa wakazi wa Dodoma na maeneo mbalimbali waendelee kushiriki katika ‘ program’ mbalimbali za elimu kwa umma ambazo zinalenga kuwaelimisha kuhusiana na umuhimu wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na nafasi za uongozi wa serikali za mitaa katika maisha yao ya kila siku na tunasema kwamba serikali za mitaa kwa sauti ya wananchi. Hivyo, wa...