WANADODOMA WASHAURIWA KUULAKI MWENGE WA UHURU TAREHE 3 OKTOBA, 2023
Na. Dennis Gondwe, DODOMA WANANCHI wa Wilaya ya Dodoma wameshauriwa kujitokeza kwa wingi kuupokea, kuushangilia na kuukimbiza Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 utakaoingia wilayani Dodoma kesho tarehe 3 Oktoba, 2023. Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani Rai hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu mapokezi ya Mwenge wa Uhuru wilayani Dodoma ofisini kwake. Alhaj Shekimweri alisema “nipende kuwafahamisha kuwa Mwenge wa Uhuru kesho tarehe 3 Oktoba, 2023 utapokelewa Wilaya ya Dodoma. Tunatarajia kuupokea Mwenge wa Uhuru pale Makutopora saa 12 asubuhi ukitokea Wilaya ya Kondoa. Utaendelea kukimbizwa katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dodoma ukikagua, kuzindua na kuweka jiwe la msingi katika miradi ya maendeleo. Wananchi wote mjitokeze kuulaki na kuushangilia Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Dodoma”. Akiongelea ratiba ya Mwenge wa Uhuru alisema kuwa Mwenge wa Uhuru utash...