Posts

Showing posts from January 17, 2025

Nyuki wa Tabora walamba Zabibu Sita

Image
Na. Asteria Frank, DODOMA Timu ya mpira wa miguu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Dodoma Jiji yainyuka goli 6-0 timu ya mpira wa miguu ya vijana wa chini ya umri wa miaka 20 ya Tabora United ndani uwanja wa Jamhuri Jiji la Dodoma katika mechi ya kwanza mzunguko wa pili wa ligi ya NBC Youth League 2024/2025. Kocha wa timu ya vijana umri wa miaka 20 ya Dodoma Jiji FC, Chido Jeremia alisema hawakuwa na mchezo mzuri kipindi cha kwanza na kipindi cha pili walikuwa na nyakati nzuri kwa jinsi vijana walivyowaelekeza kwa hali ya kuona mapungufu ya wenzao na kuweza kupata magoli hayo. Alisema kuwa timu inaendelea kuimarika na malengo waliyowawekea yanazidi kupungua maana kadri siku wanavyocheza mechi wanapata alama. “Vijana wametuheshimisha tumepata ushindi na sio tu matokeo mazuri ila matokeo yenye magoli mengi kama vile tulivyokuwa tunataka maana tulikuwa tunataka kutengeneza ‘margin’ nzuri zaidi ya wanaotufata lakini pia kutengeneza ‘goal difference’ ambayo ndio vijana wametu-off...