Posts

Showing posts from April 11, 2024

Miundombinu chachu ongezeko uandikishaji wanafunzi Jiji la Dodoma

Image
  UBORESHAJI wa miundombinu ya elimu unaoendelea kufanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan umekuwa chachu ya ongezeko la uandikishwaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza na awali Jiji la Dodoma kutoka asilimia 98 hadi 115 kwa mwaka 2024. Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mwl. Prisca Myalla Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mwl. Prisca Myalla alipokuwa akiongelea mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita kwa miaka mitatu ofisini kwake. “Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi Jiji la Dodoma tunampongeza sana Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya elimu na kutujengea shule mpya kupitia mradi wa BOOST na EP4R. Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeweza kujengewa madarasa mapya na kuboreshewa miundombinu hali iliyopelekea wazazi na jamii kuona fursa ya kuwaleta watoto wao kupata elimu. Serikali imejitahidi sana kuhakiki...