Rushwa Adui wa Haki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
Na. Coletha Charles, DODOMA Muelimishaji wa Darasa Tembezi Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Chacha Marwa amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura ifikapo tarehe 27 Novemba, 2024 katika vituo husika. Marwa alitoa elimu hiyo kwa wananchi waliopanda gari tembezi kutoka Soko la wazi la Machinga hadi Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa kuwakumbusha kuwa haki ya kiongozi bora ipo mikononi mwao. Alisisitiza kuwa kupiga kura ni msingi wa maendeleo katika mitaa yao kwa kuzingatia haki na kutokupokea rushwa ya aina yoyote kutoka kwa wagombea wa nafasi ya mwenyekiti na wajumbe watano (5) wa serikali za mitaa. “Elimu hii ni muhimu kwa wananchi wote hasa mliojiandikisha kwenye orodha ya daftari la wapiga kura, ni muhimu sana kupata haki yako ya msingi, msipoenda kupiga kura mtashindwa kupata viongozi bora wa kuleta maendeleo. Mjitahidi kuchagua viongozi wazalendo wenye busara kwa kusikiliza sera zao. Pia walemavu ambao hawezi kufika katika vituo vya kupiga kura, s...