Wanawake Dodoma watakiwa kujishughulisha
Na. Dennis Gondwe, MSALATO WANAWAKE wametakiwa kujishughulisha na shughuli za uzalishaji mali ili kuweza kukuza kipato cha familia na taifa kwa ujumla kutokana na fursa za kazi zilizopo katika Mkoa wa Dodoma. Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Dodoma, Mwl. Neema Majula akiongea na wanawake waliohudhuria Kliniki Zahanati ya Msalato Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Dodoma, Mwl. Neema Majula alipokuwa akiongea na wanawake katika maadhimisho ya siku ya wanawake Kata ya Msalato yaliyofanyika katika Zahanati ya Msalato katika Kata ya Msalato. Mwl. Majula alisema kuwa kila mwanamke katika Mkoa wa Dodoma anatakiwa kujishughulisha ili kukuza kipato cha familia na taifa. “Ndugu zangu wakati mwingine ukatili wa kijinsia unatokana na kina mama kutokujishughulisha na uzalishaji mali katika ngazi ya familia. Hivyo, unyanyasaji unakuwepo kwa sababu kila kitu unamtegemea baba alete. Nata...