BANDA YA JIJI LA DODOMA LATOA TEKNOLOJIA UFUGAJI SAMAKI NA KUKU PAMOJA
Na. Dennis Gondwe, NZUGUNI WANANCHI wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wamehamasishwa kujifunza teknolojia ya ufugaji wa samaki na kuku kwa pamoja ili kujiongezea kipato. Afisa Uvuvi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Tausi Kiula Hamasa hiyo ilitolewa na Afisa Uvuvi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Tausi Kiula alipokuwa akihamasisha ufugaji wa pamoja wa samaki na kuku kwa wananchi waliotembelea banda la mifugo la Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Kiula alisema “tunawahamasisha wananchi wote waje wajifunze katika bwawa letu hapa. Kama unavyoona teknolojia nzuri ya kisasa ambayo unapoiona unahamasika. Unachimba bwawa la samaki kisha unajenga kibanda cha kuku kwa juu yake ili kuku wakiwa wanajisaidia kinyesi kinadondoka katika bwawa la samaki na kusaidia ‘fertilization’ kwa kuweka mbolea inayobadilisha maji kuwa ya kijani na kutengeneza chakula cha samaki”. Akiongelea umuhimu wa ufugaji huo alisema kuwa unawahakikishia samaki chakula bora. “Maji yanapobadilika kwenda rangi ya k...