Miaka 63 ya Uhuru, watanzania waaswa kutunza na kuthamini Uhuru
Na. Faraja Mbise, DODOMA Watanzania wameaswa kutunza na kuthamini uhuru kwa kufanya mambo yanayoleta amani na usalama wa nchi, ili kufurahia matunda ya uhuru yaliyopatikana ndani ya miaka 63 tangu tarehe 09 Desemba, 1961. Hayo, yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, alipokuwa akizungumza na mamia ya wananchi waliohudhuria katika kilele cha Maadhimisho ya M iaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika katika makutano ya Barabara ya Mzunguko (Ring Road) katika Kata ya Makutupora, jijini Dodoma. Senyamule alisema “ i li uhuru huu tuendelee kuufurahia na kuuenzi, kwanza tuhimize amani na usalama wa nchi yetu kwasababu ni msingi wa mafanikio. Huu uhuru tunausherekea kwasababu bado tunaulinda, usije ukafikiri ukipata uhuru ndio imeisha, unaweza ukapata uhuru na baadae ukapotea tena kwasababu unaweza ukaingiliwa. Tuendelee kutunza kwa kufanya mambo ya amani na utulivu” Akizungumzia mafanikio yaliyopatikana katika Mi aka 63 ya Uhuru, aligusia mafanikio mbalimbali k...