MKOA WA DODOMA WAPATA HATI SAFI KATIKA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2023

Na. Mwandishi Maalum, KITETO Mkoa wa Dodoma wapata hati safi katika mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 baada ya miradi yake 45 kukubaliwa na katika wilaya saba na halmasahuri nane za mkoa huo. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule akitoa taarifa ya mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 Mkoani Dodoma Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule leo tarehe 7 Oktoba, 2023 wakati akikabidhi Mwenge wa Uhuru 2023 kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga katika uwanja wa Shule ya Msingi Dosidosi iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto. Senyamule akitoa taarifa ya hitimisho kwa mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 kwa Mkoa wa Dodoma, alisema kuwa Mwenge wa Uhuru ulikimbizwa kwa takribani kilometa 1893 na kupitia jumla ya miradi ya maendeleo 45. Miradi 15 iliwekewa jiwe la msingi, miradi 19 ilizinduliwa na 11 ilitembelewa yote ikiwa na jumla ya thamani ya zaidi ya shilingi Billioni 16. Miradi hiyo ni pamoja na miradi ya sekta za elimu, a...