Posts

Showing posts from August, 2026

Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akishuhudia Mhe. George Mcheche Masaju, Jaji Mkuu wa Tanzania akimuapisha, Mhe. Deogratius John Ndejembi kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino, Mkoani Dodoma, tarehe 29 Agosti, 2026.

Image
  Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akishuhudia Mhe. George Mcheche Masaju, Jaji Mkuu wa Tanzania akimuapisha, Mhe. Deogratius John Ndejembi kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino, Mkoani Dodoma, tarehe 29 Agosti, 2026.

Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza na viongozi mbalimbali kwenye hafla ya uapisho wa Mhe. Deogratius John Ndejembi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu ya Chamwino, Mkoani Dodoma tarehe 29 Agosti, 2026.

Image
  Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza na viongozi mbalimbali kwenye hafla ya uapisho wa Mhe. Deogratius John Ndejembi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu ya Chamwino, Mkoani Dodoma tarehe 29 Agosti, 2026.

Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa kwenye picha na Mhe. Deogratius John Ndejembi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya hafla ya uapisho iliyofanyika Ikulu ya Chamwino, Mkoani Dodoma tarehe 29 Agosti, 2026.

Image
  Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa kwenye picha na Mhe. Deogratius John Ndejembi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya hafla ya uapisho iliyofanyika Ikulu ya Chamwino, Mkoani Dodoma tarehe 29 Agosti, 2026.

Dodoma CC yaangukia msindi wa pili Mpira wa Wavu Wanaume SHIMISEMITA

Image
Na. Leah Mabalwe, MBEYA   TIMU ya Mpira wa Wavu ya Wanaume kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeibuka mshindi wa pili katika mashindano ya Fainali za SHIMISEMITA, baada ya kukubali kichapo cha Seti 3-0 kutoka kwa Manispaa ya Iringa katika mchezo wa fainali uliochezwa kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Samora.   Mchezo huo wa fainali ulikuwa wa ushindani mkubwa, huku timu zote zikionesha kiwango kizuri cha mchezo na kupambana kutwaa ubingwa wa mashindano hayo. Kocha wa Timu ya Mpira wa Wavu ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Wanjala Matinya alisema kuwa timu yake ilijiandaa vizuri hadi kufikia hatua ya fainali, lakini pia wapinzani wao walikuwa wamejiandaa ipasavyo na kuweza kupata ushindi.   “Tumejiandaa vizuri hadi kufikia hatua ya fainali. Lakini wapinzani wetu nao walikuwa wamejiandaa vizuri, ndiyo maana wameweza kupata ushindi” alisema Matinya. Kwa upande wake, mchezaji wa Timu ya Mpira wa Wavu, Galucy Kyando alisema kuwa mchezo huo ulikuwa wa ushindani...

Baraza la Madiwani Jiji la Dodoma lampongeza Ndejembi kuteuliwa Makamu wa Rais

Image
Na. Coletha Charles, DODOMA   Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma limempongeza Waziri wa Nishati na Mbunge wa Jimbo la Chamwino, Deogratius Ndejembi kwa kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) tarehe 26 Agosti 2026.   Pongezi hizo zilitolewa na Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Bakari Fundikira wakati akiongoza Baraza maalum la Madiwani kwa ajili ya kupokea taarifa ya ufungaji wa hesabu za Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa mwaka ulioishia tarehe 30 Juni, 2026 katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.   Fundikira alisema kuwa Baraza zima la Madiwani linampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumteua Deogratius Ndejembi kushika nafasi hiyo ya Makamu wa Rais, huku akimtakiwa heri katika utekelezaji wa majukumu yake mapya.   “Lakini pia tutumie nafasi hii kumpongeza Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa u...

IPSIS yawarahisishia madiwani Dodoma kufanya maamuzi

Image
Na. Lulu Luvanda, DODOMA Mfumo wa Kimataifa wa Uandishi na Uwasilishaji wa Taarifa za Fedha (IPSIS) umeelezwa kuwa umepunguza ugumu wa uandishi na uchakataji wa taarifa za fedha katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, huku ukirahisisha uwasilishaji wa hesabu na kuwawezesha madiwani kufanya maamuzi kwa uelewa zaidi.   Akizungumza wakati wa mkutano maalumu wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma ililofanyika katika ukumbi wa mikutano ya halmashauri Diwani wa Kata ya Miyuji, Ringo Iringo alisema kuwa   mfumo huo ni muhimu kwa Jiji la Dodoma kutokana na shughuli nyingi za kiuchumi na miradi mbalimbali ya maendeleo na ongezeko la shughuli za kifedha zinazohitaji usimamizi madhubuti. Alisema kuwa mfumo wa IPSIS umeleta urahisi katika uandishi na uwasilishaji wa taarifa za kifedha, pamoja na kufanya mchakato wa kuchakata taarifa kuwa mwepesi na hivyo kusaidia viongozi kupata taarifa zinazoweza kuwa msingi wa kufanya maamuzi kwa wakati. “Kwa sababu hiyo, IPSIS ni ...

Baraza la Madiwani Jiji la Dodoma lapitisha taarifa ya ufungaji hesabu 2025/2026

Image
Na. Manase Malima, DODOMA Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma limeridhia na kuthibitisha taarifa ya ufungaji wa hesabu za halmashauri za hadi kufikia tarehe 30 Juni, 2026 huku madiwani wakisisitiza umuhimu wa kuendeleza uwazi na uwajibikaji katika uongozi na usimamizi wa fedha za umma. Taarifa hiyo iliwasilishwa katika mkutano maalum wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, ambapo Mkuu wa kitengo cha Fedha na Uhasibu, CPA. David Rubibira aliwasilisha taarifa hiyo kwa ajili ya kuhakikiwa na kuthibitishwa na baraza. CPA. Rubibira alisema kuwa taarifa za ufungaji wa hesabu za halmashauri kwa tarehe 30 Juni, 2026 ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa kuwasilisha taarifa za kifedha kwa ajili ya kuhakikisha kuwa taarifa za halmashauri zinaakisi hali halisi ya matumizi na usimamizi wa fedha. Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Zuzu, Jenesta Malingo alisema kuwa ameridhishwa na taarifa hiyo na anaamini kuwa uwazi katika uwasil...

Wilaya ya Dodoma kuchanja watoto zaidi ya laki 2 chanjo ya Polio

Image
Na. Coletha Charles, NKUHUNGU   Wilaya ya Dodoma imejipanga kuchanja watoto 207,096 chini ya miaka 10 dhidi ya ugonjwa wa Polio, sawa na asilimia 21 ya lengo la mkoa mzima, ikiwa ni utekelezaji wa kampeni ya kitaifa ya kujikinga na mlipuko wa ugonjwa huo. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, iliyofanyika katika Shule ya Msingi Nkuhungu, Kata ya Nkuhungu Halmshauri ya Jiji la Dodoma Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri alisema kuwa wilaya hiyo imekamilisha maandalizi yote ya kimkakati kupitia vikao vya ngazi tatu wataalamu, makundi ya hamasa na Kamati ya Afya ya Msingi ya Wilaya. “Waliopewa kazi ya kuhamasisha, wafanye kazi hiyo ya uhamasishaji kikamilifu. Na kwa bahati njema, kama ambavyo tumeona hapa, wanatoka kwenye ngazi ya jamii, kwa hiyo wanafahamu namna ya kushirikiana na jamii. Tumepewa lengo la kuchanja watoto 207,096,” alisema Alhaj Shekimweri. Alitumia nafasi hiyo kubainisha kuwa nchi haina mgonjwa wa Polio kwa sasa, hatua hiyo ni maelekezo ...

Wilaya ya Dodoma kutumia vyombo vya habari katika kampeni ya dhidi ya chanjo ya Polio

Image
Na. Coletha Charles, NKUHUNGU Wilaya ya Dodoma imeweka mkakati wa kutumia vyombo vya habari, viongozi wa dini, shule na kampuni za simu ili kuwahamasisha wazazi kuwapeleka watoto kupata chanjo salama dhidi ya ugonjwa wa Polio, lengo likiwa ni kutokomeza kabisa hatari ya maambukizi ya ugonjwa huo. Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa zoezi hilo katika Shule ya Msingi Nkuhungu, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri, alisema kuwa vipindi vya redio na televisheni, hususani vipindi vya asubuhi, vitatumika kutoa elimu kwa wananchi na kujibu maswali kuhusu umuhimu na usalama wa chanjo hiyo. Alisema kuwa viongozi wa dini nao wamepewa nafasi muhimu katika uhamasishaji huo, kutokana na ushawishi wao katika jamii na uwepo wa watoto katika maeneo ya ibada, ikiwemo ‘Sunday Schools’, madrasa na jumuiya mbalimbali za kidini. “Tumeona pia kupitia eneo hilo kila mtoto wa Tanzania apate nafasi ya kupata chanjo hiyo. Tumewahamasisha shule zote, kamati na bodi za shule kufikisha ujumbe...

Tarura Dodoma yatakiwa kukamilisha miradi kwa wakati

Image
 

Wanafunzi Kizota S/M wapatiwa chanjo dhidi ya Polio

Image
Na. Jesca Kipingu, KIZOTA   Wataalamu wa afya kutoka Kituo cha Afya Kizota wamefika katika Shule ya Msingi Kizota, Kata ya Kizota, Halmashauri ya Jiji la Dodoma, kwa ajili ya kutoa chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri wa kuanzia miezi 0 hadi miaka 10, ikiwa ni sehemu ya kampeni inayoendelea ya kuwakinga watoto dhidi ya ugonjwa huo na madhara yake, ikiwemo ulemavu wa kudumu. Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Katibu wa Afya katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma ambaye pia ni Msimamizi wa Kampeni ya Chanjo ya Polio, Hapiness Kaungya, aliwashukuru wazazi kwa mwitikio mkubwa walioonesha katika kuhakikisha watoto wao wanapatiwa chanjo. Alisisitiza kuwa ushiriki wa wazazi na walezi ni muhimu katika kuhakikisha watoto wanapata kinga dhidi ya ugonjwa wa Polio.   Aidha, Kaungya aliitaka jamii kuendelea kupata na kuzingatia taarifa sahihi zinazotolewa na wataalamu wa afya ili kuondokana na dhana potofu kuhusu chanjo. Alisema kuwa ushirikiano wa wazazi, walezi na jamii kwa ujumla ...

Bwawa kujengwa kudhibiti mafuriko Nzuguni, Dodoma

Image
 

DC Dodoma aagiza utambuzi wa kaya maeneo hatarishi

Image
 

DC Shekimweri aagiza kuzingatia usalama maeneo ya uchimbaji madini

Image
 

DC Dodoma aagiza Kampeni Maalumu ya Usafi kukabiliana na El Nino

Image
 

Kampeni dhini ya Polio yashika kasi Dodoma

Image
 

Watoto chini ya Miaka 10 wakipatiwa Chanjo ya Polio

Image
 

RC Senyamule azindua Kampeni ya Chanjo ya Polio Dodoma

Image
 

Wazazi wahimizwa kuwapeleka watoto kupata chanjo ya Polio

Image
Na. Josephina Kayugwa, DODOMA   Serikali imejipanga kuhakikisha watoto wanapatiwa chanjo ya Polio ili kuendelea kuilinda Tanzania dhidi ya ugonjwa huo, licha ya nchi kutokuwa na mgonjwa wa Polio kwa sasa. Hayo aliyasema Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri katika hafla fupi ya ufunguzi wa kampeni ya utoaji chanjo ya Polio iliyofanyika katika Shule ya Msingi Nkuhungu, Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Alhaj Shekimweri alisema kuwa hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za serikali chini ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuimarisha afya za watoto nchini, akieleza kuwa watoto wamekuwa sehemu muhimu ya programu mbalimbali za afya zinazotekelezwa na serikali. Aliongeza kuwa kama Wilaya ya Dodoma imepewea lengo la kuwafikia watoto 207,096 katika zoezi hilo, ikiwa ni sehemu ya jumla ya watoto 1,003,061 katika Mkoa wa Dodoma wanaolengwa katika maeneo husika. “Viongozi, watendaji wa serikali, shule, kamati na bodi za shule wamehamasishwa kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo, i...

TARURA Dodoma yatakiwa kukamilisha miradi kwa wakati

Image
Na. Coletha Charles, NZUGUNI Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA) wametakiwa kukamilisha kwa wakati, miradi ya uboreshaji wa barabara yenye urefu wa kilomita 3.8 kwa kuzingatia ubora na thamani ya fedha ili iweze kuleta manufaa yaliyokusudiwa kwa wananchi wa Jiji la Dodoma.   Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri, wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya mradi huo, ikiwa ni sehemu ya hatua za kukabiliana na athari za mvua za El Nino. Alisema kuwa utekelezaji wa mradi huyo unapaswa kwenda sambamba na usimamizi madhubuti wa muda, ubora wa kazi na matumizi sahihi ya fedha, ili wananchi wa Jiji la Dodoma wanufaike na miundombinu hiyo kwa muda uliokusudiwa. “Ninawasihi TARURA kuhakikisha mradi huu unakamilishwa kwa wakati na kwa kuzingatia viwango vinavyotakiwa, ili wananchi waweze kupata manufaa yaliyokusudiwa. Muhimu ni kuhakikisha fedha zinazotumika katika mradi huu zinatoa thamani halisi kwa wananchi,” ...

Bwawa kujengwa kudhibiti mafuriko Nzuguni

Image
Na. Coletha Charles, NZUGUNI Ujenzi wa bwawa kubwa la kuhifadhi maji ya mvua pamoja na mtaro wenye urefu wa zaidi ya kilomita 3.6 umeanza kutekelezwa katika Uwanja wa Maonesho ya Nanenane wa Dkt. John Malecela, hatua inayolenga kudhibiti mafuriko katika eneo la Nzuguni na kuyageuza maji hayo kuwa fursa ya uzalishaji.   Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi huo katika Kata ya Nzuguni jijini hapa, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabiri Shekimweri alisema kuwa serikali imejipanga kukabiliana na changamoto ya mafuriko katika eneo hilo, huku ikilenga kutumia maji ya mvua kwa kilimo na uvuvi.   Alisema kuwa kwa wastani Dodoma hupokea mvua kati ya milimita 440 na 550 kwa mwaka, hivyo kuna umuhimu wa kuweka mifumo ya kuvuna na kuhifadhi maji badala ya kuyaacha yapotee.   “Bwawa hili litapokea na kuhifadhi maji yanayokusanywa kutoka maeneo yanayozunguka uwanja na hivyo kupunguza hatari ya mafuriko kwa wananchi wa maeneo jirani. Pia mpango huu umez...

DC Shekimweri aagiza utambuzi wa kaya maeneo hatarishi

Image
Na. Coletha Charles, NZUGUNI Idara ya Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Jamii, Madiwani, Watendaji wa Kata na Polisi Kata, wameagizwa kushirikiana na mamlaka nyingine kubaini kaya zinazoishi katika maeneo hatarishi, ikiwemo njia za asili za maji, yanayoweza kuhatarisha usalama wa maisha na mali za wananchi na kuzihamasisha kuhamia katika maeneo salama. Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri katika Jengo la Utawala la Viwanja vya maonesho ya Nanenane vya Dkt. John Malecela Kata ya Nzuguni, wakati wa utekelezaji wa maelekezo ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu kuchukua hatua za kuzuia na kupunguza athari za mvua za El Nino pamoja na mvua zitakazokuwa juu ya wastani.   Alisema kuwa baadhi ya wananchi wamekuwa wakijenga katika njia za asili za maji, hususan wakati wa kiangazi, jambo ambalo linaweza kuhatarisha maisha na mali wakati wa mvua, ambapo maji hurejea katika mikondo yake ya kawaida.   “Ujenzi katika maeneo hatarishi hauathiri ...