Posts

Showing posts from May, 2026

JIJI LA DODOMA LATOA VIWANJA 1,900 KWA WAFANYAKAZI

Image
  Na. Mwandishi wetu, DODOMA HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imeibuka kivingine katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani kwa kuachia viwanja zaidi ya 1,900 vya matumizi mbalimbali kwa ajili ya wafanyakazi na wananchi kwa ujumla ili waweze kufurahia fursa ya kumiliki kiwanja katika makao makuu ya nchi. Kauli hiyo ilitolewa na Katibu wa Baraza la Wafanyakazi la Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dennis Gondwe alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu nafasi ya Halmashgauri ya Jiji la Dodoma katika kujali makazi ya wafanyakazi katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika ngazi ya mkoa katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. “Nitumie nafasi hii kuwashauri na kuwashawishi wafanyakazi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma na wengine wote kuhakikisha wananunua viwanja katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Hii itaweka alama kwa utumishi wao katika halmshauri, lakini kwa wale walio nje ya halmshauri itaweka alama kwa kumiliki kiwanja kihalali katika makao makuu...