Posts

Showing posts from April 26, 2025

Shekimweri awapa maua yao Vijana Wilaya ya Dodoma

Image
Na. Mussa Richard. DODOMA Mkuu wa Wilaya ya Dodoma , Alhaj . Jabir Shekimweri amewapongeza v ijana walioshiriki katika Kongamano la Mwenge wa Uhuru la vijana 2025 lililofanyika katika u wanja w a Shule ya Msingi Mbwanga jijini Dodoma. Aliyasema hayo wakati akimkaribisha Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025, Ndugu Ismail Ussi wakati wa kufunga Kongamano la Mwenge wa Uhuru la vijana. “Nimefarijika kuona vijana wamejitokeza kwa wingi na kushiriki ipasavyo katika mada mbalimbali ambazo zimewasi l ishwa na watoa mada pamoja na wachombeza mada . Pia n iwatoe wasiwasi vijana wote walioshiriki katika k ongamano hili kuwa mapendekezo yao nimeyapokea na nitayafanyia kazi ili kuhakikisha vijana katika Wilaya ya Dodoma wanajikwamua kimaisha kwa kutatuliwa kwa baadhi ya changamoto ambazo zinawakabi l i ” alisema Alhaj . Shekimweri. Katika hatua nyingine aliwapongeza watoa mada na wachombeza mada wote walioshiriki katika kutoa mada na mafunzo mbalimbali kwa vijana katik...

Vijana watakiwa kuchangamkia fursa mbalimbali ili kujikwamua kiuchumi

Image
Na. Leah Mabalwe, MNADANI Mwakilishi wa Kampuni ya MAINLAND inayojenga Kiwanda cha kutengeneza mafuta ya Alizeti, Fadhili Makenjula awataka vijana kujitokeza katika nafasi za kazi mbalimbali zitakazotangazwa na kiwanda hicho cha Mafuta kitakapo kamilika mwezi Juni, 2025 ili kujikwamua kiuchumi. Mwakilishi wa Kampuni ya MAINLAND inayojenga Kiwanda cha kutengeneza mafuta ya Alizeti, Fadhili Makenjula Aliyazungumza hayo kwenye Kongamano la Vijana katika Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2025 lililofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Mbwanga jijini Dodoma. Alisema kuwa vijana wanapaswa kuchangamkia fursa bila kuchagua kazi ili kujikwamua kiuchumi. “Nipende kuwataarifu kuwa, tupo katika hatua ya umaliziaji wa ujenzi wa kiwanda kikubwa cha mafuta ya alizeti kilichopo Kata ya Msalato, Mtaa wa Veyula. Vijana jitokezeni kwa wingi katika kutuma maombi ya kazi, kuna vitengo mbalimbali katika kiwanda hicho. Wewe kama kijana usiogope kuleta maombi yako kwaajili ya nafasi ya kazi. Tunawapa vija...

Mzee Bukitu aongelea Falsafa ya Mwenge wa Uhuru kwa Vijana Dodoma

Image
Na. Nancy Kivuyo, MNADANI Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation, Mzee Joseph Butiku amesema falsafa ya Mwenge wa Uhuru ilianzishwa kwa lengo la kuleta upendo na mshikamano kwa taifa huku mwanga wa Mwenge ukiangazia mipaka ili kuleta matumaini palipo kukata tamaa, upendo palipo uadui na heshima palipo chuki. Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation, Mzee Joseph Butiku akielezea Falsafa ya Mwenge wa Uhuru Aliyasema hayo katika Kongamano la Mwenge wa Uhuru la Vijana 2025 lililofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Mbwanga. Alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 1958 Mwalimu Nyerere alianzisha falsafa hiyo kipindi cha jitihada za kupata uhuru. “Niwaeleze kuwa, Mwenge wa Uhuru ni kielelezo cha amani na matumaini. Wakati sisi tunapata ufahamu kuhusu Mwenge, tuliingiwa na uzalendo wa hali ya juu ndio maana mnaona taifa letu lipo imara hadi leo” alisema Mzee Butiku. Aliongeza kuwa vijana wa kizazi cha leo wanapaswa kuisoma historia ya Mwenge wa Uhuru kwa mapenzi ...

Wilaya ya Dodoma mtekelezaji kinara Agenda ya Nishati safi ya kupikia

Image
Na. Dennis Gondwe, NALA WILAYA ya Dodoma imekuwa ikitekeleza maagizo na falsafa ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa vitendo katika utekelezaji wa dhamira yake ya nishati safi. Kauli hiyo ilitolewa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde alipokuwa akisalimia mamia ya wananchi wa Jiji la Dodoma waliojitokeza kuulaki Mwenge wa Uhuru ulipotembelea Shule ya Sekondari ya Wasichana Santhome - SABS kutembelea mradi wa nishati safi ya kupikia. Mavunde alisema kuwa Wilaya ya Dodoma ipo mstari wa mbele kutekeleza maagizo na falsafa ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa vitendo ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi. ”Mheshimiwa mkuu wa wilaya ninakushukuru sana kwa kusimamia kikamilifu na kuhakikisha taasisi na shule mbalimbali zinafunga mfumo wa nishati safi ya kupikia. Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Mwaka 2025, Wilaya ya Dodoma ni kati ya wilaya kielelezo kwa nchi yetu katika kutekeleza falsafa ya rais wetu” alisema Mavunde. Akisoma taarifa ya mradi wa ni...

Mwenge wa Uhuru waridhishwa na ujenzi wa Barabara yenye urefu wa KM 1.6 kiwango cha lami

Image
Na. Dennis Gondwe, NALA MWENGE wa Uhuru Mwaka 2025 umeridhishwa na kiwango cha ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 1.6 kwa kiwango cha lami kutoka barabara iendayo Singida hadi Hospitali ya Jiji la Dodoma inayojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 2.8. Kauli hiyo ilitolewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Mwaka 2025, Ismail Ussi alipokuwa akiongea na wananchi wa Kata ya Nala na maeneo ya jirani waliojitokeza kwa wingi kuupokea na kuushangilia Mwenge wa Uhuru Mwaka 2025 uliotembelea ujenzi wa barabara hiyo. Alisema kuwa Mwenge wa Uhuru ni ishara ya matumaini, upendo, heshima, amani na maendeleo chini ya serikali ya awamu ya sita. “Leo tumekuja kujionea ujenzi wa barabara ya kisasa yenye ubora, inayojengwa na serikali ya awamu ya sita, inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kilometa 1.6 kwa kiwango cha lami. Wananchi wa kata waliomba barabara hii kupitia mbunge na diwani wao. Barabara hii itasaidia wananchi wanapoenda kupata huduma za afya katika Hosp...

Mwenge wa Uhuru kutembelea miradi 7 ya shilingi Bil. 11.1 Dodoma

Image
Na. Dennis Gondwe, CHIGONGWE MWENGE wa Uhuru Mwaka 2025 utatembelea miradi saba ya maendeleo yenye gharama ya shilingi bilioni 11.1 iliyotekelezwa kwa ajili ya kuwapelekea maendeleo na kuboresha maisha ya wananchi katika Wilaya ya Dodoma. Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri (kushoto) wakati akipokea Mwenge wa Uhuru Mwaka 2025 kutoka kwa Mkuu wa Wilaya Bahi Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri wakati akipokea Mwenge wa Uhuru Mwaka 2025 kutoka kwa Mkuu wa Wilaya Bahi tukio lililofanyika katika uwanja wa Ofisi ya Afisa Mtendaji Kata ya Chigongwe jijini Dodoma. Shekimweri alisema kuwa Mwenge wa Uhuru Mwaka 2025 ukiwa katika Wilaya ya Dodoma utachochea maendeleo. “Mimi Jabir Mussa Shekimweri, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, nakiri kuupokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mheshimiwa Joachim Nyingo ukiwa unawaka, unang’aa na unameremeta. Aidha, nakiri kuwapokea wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa wakiwa na afya njema. Mwenge wa Uhuru ukiwa...