Shule ya Sekondari ya Bil. 3.9 kujengwa Kata ya Chahwa
Na. Emanuel Charles, CHAHWA Hafla ya kusaini Mkataba wa Ujenzi wa Shule ya Sekondari Chahwa wenye thamani ya shilingi bilioni 3.9 baina ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma na Mkandarasi kutoka Gopa contractors Tanzanian Limited imefanyika katika Kata ya Chahwa ukilenga kusogeza huduma ya elimu karibu na wananchi. Mradi huo unatekelezwa kwa mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma ukiwa ni ujenzi wa shule ya ghorofa nne yenye madarasa 12, maktaba pamoja na maabara nne, chumba cha TEHAMA na jengo la utawala na unatarajiwa kukamilika ndani ya mwaka mmoja. Akizungumza katika utiaji saini wa ujenzi wa shule hiyo Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde alitoa pongezi kwa serikali kwa kuendelea kuboresha sekta ya elimu na kuleta miradi mikubwa katika maeneo ya nje ya Mji wa Dodoma. “Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa mradi huu mkubwa kwasababu unaenda kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya elimu, ndugu zangu ni wakati sasa maeneo ya pembezoni mwa Jiji la Dodoma yanufaike...