Na. Nancy Kivuyo, MATUMBULU MIKOPO isiyo na riba ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu imekuwa chachu ya kusukuma maendeleo katika sekta za kilimo, ufugaji na ujasiriamali. Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea kikundi hicho kufuatilia manufaa ya mikopo hiyo kwa jamii, Mwenyekiti wa Kikundi cha Kilasara, Judika Urio alisema kuwa wanawake hao wamenufaika na mkopo huo usio na riba. āKikundi chetu tupo watano, tulipata takribani shilingi milioni 20 ambazo tuliwekeza katika ufugaji wa kuku, bata mzinga, bata bukini na sungura. Baada ya mafanikio ya ufugaji huo, tulipata faida ambayo ilituwezesha kuanzisha mradi mwingine wa uzalishaji wa samaki kama mnavyoona kwenye mabwawa haya, tumeweka mbegu ya samaki wapatao elfu 10 ambao tunategemea baada ya mwaka ndio tuvuneā alisema Urio. Alimshukuru Rais, kwa kuyajali makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, na kusema kuwa amewainua ...