ASMA KARAMA ACHAGULIWA NAIBU MEYA JIJI LA DODOMA

Na. Dennis Gondwe, DODOMA ASMA Said Karama amechaguliwa kwa asilimia 100 kuwa Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri. Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Asma Said Karama Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Mwenyekiti wa Uchaguzi wa Naibu Meya, Sakina Mbugi alisema āMheshimiwa Asma Said Karama amepata kura 55 sawa na asilimia 100 ya kura zote zilizopigwa na wajumbe. Kwa mamlaka niliyopewa ninamtangaza Mheshimiwa Asma Said Karama kuwa Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodomaā. Akitoa neno la shukrani Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Asma Karama alisema alimshukuru Mungu kwa baraka zake. āNapenda kukishukuru chama changu cha Mapinduzi kwa kuniruhusu kuingia kinyangāanyiro hiki. Kipekee zaidi napenda kuwashukuru madiwani kwa kuniamini na kunituma ili niwatumikie, tufanye kazi pamoja na kumsaidia Mstahiki Meya na kuwaletea maendeleo wana Dodoma. Kipekee zaidi nashukuru ...