DC Shekimweri asisitiza urasimishaji biashara za wanawake
Na. Paulo Paulo, VIWANDANI Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri ametoa rai kwa wanawake wajasiriamali kutumia vema fursa ya uwepo wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi ili kukuza biashara zao na kuchangia katika maendeleo ya uchumi wa taifa. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Wilaya ya Dodoma, aliwapongeza viongozi wapya waliochaguliwa na kuwataka kutekeleza majukumu yao kwa tija, uadilifu na ushirikiano mkubwa na serikali pamoja na mamlaka husika. Sambamba na hilo aliwataka wajasiriamali kurasimisha biashara zao ili kuongeza fursa za kutambulika, kupata masoko mapya, na kufaidika na fursa za uwekezaji na mikopo pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuendelea kutoa elimu, ushauri, na kujenga mahusiano mazuri na wafanyabiashara wadogo badala ya kulenga ukusanyaji wa kodi pekee. Aliwahimiza wanawake kutumia teknolojia ya kidijitali na mifumo ya kisasa katika kutafuta masoko na kusimamia fedha za ...