Wananchi 2,700 Kunufaika, Mradi wa Ukarabati Maji Taka
Na. Faraja Mbise, KIWANJA CHA NDEGE Takribani wakazi 2,700 wanatariwa kunufaika na mradi wa ukarabati wa mtandao wa maji taka unaotekelezwa na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) katika Mtaa wa Area C na D, Kata ya Kiwanja cha Ndege, jijini Dodoma. Hayo yalisemwa na Mhandisi wa Maji taka DUWASA, Mhandisi Yohana Koroso alipokuwa anawasilisha taarifa ya mradi wa ukarabati wa mtandao wa Maji taka katika eneo la Area C na D wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Dodoma. Mhandisi Koroso alisema āmradi unagharimu jumla ya shilingi bilioni 4.9 ambao utawezesha jumla ya watu 2,700 kunufaika na mradi huo katika uondoaji wa Maji takaā. Akizungumza wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Dodoma, alisema ukarabati wa miundombinu ya Maji taka una urefu wa Kilomita 19 za mabomba ya plastiki (PVC). Mhandisi Koroso alisema āukarabati wa miundombinu ya maji taka maeneo ya Area C na D wenye urefu wa Kilom...