Posts

Showing posts from February 27, 2026

Shule ya Msingi Mazengo ipo moto

Image

Huduma ya Lishe kwa Shule za Dodoma

Image
 

Stadi za Maisha Kuwa mkombozi kwa wanafunzi wa Sekondari jijini Dodoma

Image
Na. Mwandishi Wetu, DODOMA Elimu ya Stadi ya Maisha imetajwa kuwa ni chachu ya mabadiliko chanya kwa wanafunzi katika kuwajengea uwezo wa kujitambua na kukabiliana na changamoto za maisha katika shule za sekondari jijini Dodoma. Hayo aliyasema Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Daniel Mapilya wakati akifungua mafunzo kwa wawezeshaji wa stadi za maisha katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Dodoma. Alieleza kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha wawezeshaji wanapata uelewa wa kutosha juu ya namna bora ya kuwafikia wanafunzi na kuwajengea misingi imara ya maisha. “Tunapozungumzia stadi za maisha, tunalenga kumsaidia mwanafunzi kujitambua, kujiamini na kufanya maamuzi sahihi. Elimu hii itawawezesha vijana wetu kuepukana na vishawishi vinavyoweza kuathiri masomo na mustakabali wa maisha yao” alisema Mapilya. Aliongeza kwa kusema kuwa changamoto nyingi zimekuwa zikiwakumba watoto wa kike. ”…zikiwemo shinikizo la rika na mazingira yasiyo rafiki, hivyo elimu hiyo it...

Utatuzi mgogoro wa Mahomanyika watangazwa

Image
Na. Nancy Kivuyo , NZUGUNI Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeunda timu mbili ya wataalam wa upangaji na upimaji na timu ya uhakiki kwaajili ya kutatua mgogoro wa ardhi wa muda mrefu katika eneo la Mahomanyika. Timu hizo zimeundwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Leonard Akwilapo alipokuwa akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Mahomanyika, Kata ya Nzuguni jijini Dodoma. Alisema kuwa timu hizo zitaanza kazi mara moja ili kuhakikisha zoezi hilo linakamilika kwa wakati. “Eneo la Mahomanyika ni la serikali kwahiyo , naagiza lipangwe na kupimwa kwaajili ya kutatua mgogoro huu na kuwa kielelezo cha utatuzi wa migogoro mingine iliyopo ndani ya Jiji la Dodoma. Timu hizi zinapaswa kufanya kazi ndani ya siku 60 na kukamilisha zoezi hili ili kila mmoja ajue amepata nini na anaenda wapi” alisema Dkt. Akwilapo. A liongeza kuwa wale wote waliohusika kwenye kadhia ya mgogoro huo wa ardhi watachukuliwa kwaajili ya maho...

Timu ya ‘sustainability’ ya Jiji la Dodoma yaanza semina ya siku saba

Image
  Na. Nancy Kivuyo , DODOMA Mafunzo maalum kuhusu viwango vipya vya uhasibu ‘ General Requirements for Disclosure of Sustainability-related Financial Information na Climate-related Disclosures’ (IFRS S1 na IFRS S2) yameanza rasmi kutolewa kwa timu ya ‘sustainability’ ikiwa ni sehemu ya mpango wa mafunzo ya uendelevu ‘sustainabilty and ESG’ yanayolenga kuwajengea uelewa na kuongeza ufanisi katika usimamizi wa taarifa za kifedha. Akizungumza wakati wa semina hiyo ya siku ya kwanza, Mratibu wa Mafunzo ya ‘sustainability’ katika Jiji la Dodoma, Akida Huddu alisema kuwa mafunzo hayo yamelenga kutoa elimu ya jumla ya uendelevu ‘sustainability and ESG’ kwa washiriki ili kuwawezesha kusimamia kwa ufanisi shughuli zote zinazohusiana na uendelevu pamoja na kupata taarifa zitakazosaidia kutoa huduma nzuri kwa wananchi. Aliongeza kuwa uelewa wa viwango vipya vya uhasibu ni muhimu katika kuimarisha uwazi, uwajibikaji na usimamizi bora wa rasilimali za umma, hususan katika mazingira yanayoh...

Wawezeshaji Stadi za Maisha watakiwa kuwa na nidhamu na uwajibikaji

Image
Na. Mwandishi Wetu, DODOMA Wawezeshaji wa Stadi za Maisha katika Shule za Sekondari Jiji la Dodoma wametakiwa kuwa na nidhamu ya hali ya juu katika mazingira ya shule watakazopangiwa pamoja na kutumia mafunzo waliyoyapata kwa kuleta mabadiliko chanya kwa wanafunzi. Hayo yalisemwa na Mwezeshaji mafunzo y a Stadi za Maisha wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Tuvacal Mjema, wakati wa mafunzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Dodoma jijini Dodoma. Alisema kuwa wawezeshaji wanapaswa kuwa mfano bora kwa wanafunzi kwa kuzingatia maadili, kuwajibika ipasavyo na kuonyesha weledi katika utekelezaji wa majukumu yao. “Ni muhimu kwa wawezeshaji kuwa na nidhamu ya hali ya juu wanapokuwa shuleni. Tunapaswa kuishi yale tunayowafundisha wanafunzi ili waweze kutuamini na kufuata miongozo tunayowapatia kwasababu ninyi ndio taa yao   inayo waangazia” alisema Mjema. Lakini pia aliongezea kwa kusema kuwa mafunzo hayo yamelenga kuwaongezea uwezo wa kitaaluma na kisaikolojia wawezesh...