Posts

Showing posts from December 24, 2023

Jiji la Dodoma lasafisha korongo la Kishoka kuondoa kero ya mafuriko kwa wananchi

Image
Na. Dennis Gondwe, CHANG’OMBE HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imesikia kilio cha wakazi wa Mtaa wa Kishoka, Kata ya Chang’ombe cha kero ya kuziba kwa korongo linalopitisha maji ya mvua na kusababisha mafuriko katika makazi yao. Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Ally Mfinanga akiongelea zoezi la kuondoa taka katika korongo la Mtaa wa Kishoka Katika utatuzi wa kero hiyo Halmashauri ya Jiji la Dodoma imepeleka mtambo (JCB Backhoer) kwa ajili ya kufukua korongo hilo na kuondoa taka ngumu zilizotupwa kwenye korongo na kusababisha maji ya mvua kushindwa kupita. Akiongea wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Ally Mfinanga alisema kuwa lengo la zoezi la kusafisha korongo hilo ni kuyawezesha maji ya mvua yaweze kupita vizuri na kutosababisha mafuriko katika makazi ya watu. ā€œKama mnavyoona hapa tunaendelea na shughuli ya siku tatu ya usafishaji wa korongo la maji ya mvua katika Mtaa wa Kishoka, Kata ya Chang’ombe. Lengo kubwa ni...

Jiji la Dodoma kuendelea kusafisha makorongo ya maji ya mvua kuzuia mafuriko katika makazi ya wananchi

Image
Na. Dennis Gondwe, CHANG’OMBE HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma itaendelea kuyafanyia usafi kwa kuondoa taka ngumu makorongo yote ili yaweze kupitisha maji vizuri na kuondoa kero ya mafuriko wakati mvua zinaponyesha. Mkuu wa Kitengo cha usafi na uthibiti wa kata ngumu, Dickson Kimaro akielezea ukubwa wa kazi ya kusafisha kongoro na kuondoa taka ngumu katika Mtaa wa Kishoka Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Kitengo cha usafi na uthibiti wa kata ngumu, Dickson Kimaro alipokuwa akiongelea mipango ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika kuhakikisha wananchi hawaathiriki na mafuriko yatokanayo ma maji ya mvua kushindwa kupita kwenye makorongo. Kimaro alisema ā€œHalmashauri ya Jiji la Dodoma itaendelea kuyafanyia kazi kwa lengo la kuhakikisha wananchi hawapati kero kama hizi zinazoonekana. Kama mnavyoona kule mbele kuna eneo ambalo maji yakifika darajani yanagota na kurudi kuingia katika makazi ya watu. Hapa Mtaa wa Kishoka tunasafisha korongo hili kwa kuondoa taka ngumu na kuliongezea kina il...