Mkoa wa Dodoma kinara Mazingira ya Uwekezaji
Na. Asteria Frank, DODOMA Mkoa wa Dodoma umeibuka kinara kwa kuwa mkoa wa kwanza kupokea tuzo za uwekezeji na utengenezaji wa mazingira wezeshaji ya biashara kutoka kwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Tuzo hiyo imekabidhiwa na Mwenyekiti wa āChember of Commerceā (TCCIA) kwa Mkuu wa Mkoa Dodoma, Rosemary Senyamule katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa niaba ya Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 7 Oktoba, 2024. Senyemale alisema kuwa kupokea tuzo hiyo ni heshima kubwa sana na inahamasisha namna ya kuendelea kuboresha mazingira wezeshaji ya biashara kila siku. āSisi kwa Mkoa wa Dododma tunajua tunazo fursa nyingi lakini pia tunao wafanyabiashara wengi kwa vitengo mbalimbali na tunashukuru kuwa tuzo hizi tunazipata sio kwa Serikali ya Mkoa kusema sisi tunafanya vizuri, Tuzo hizi zinatolewa baada ya wafanyabiashara wenyewe kusema tunaonaje huduma tunazo zipata kutoka serikaliniā alisema Senyamule. Aidha, Mwenyekiti wa TCCIA Dodoma, Vivian Komu, alitoa ta...