RAIS, DKT SAMIA ATOA BIL 4.5 KULIPA FIDIA WANANCHI DODOMA

Na. Dennis Gondwe, DODOMA RAIS, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi bilioni 4.5 kwa ajili ya kulipa fidia wananchi 469 wa maeneo mbalimbali katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo alipokuwa akiongelea mafanikio ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa Uzinduzi wa Mikutano ya Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Waandishi wa Habari katika kampeni ya Tumekusikia Tumekufikia uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma. Kayombo alisema “Mheshimiwa Rais kwa upendo wake ameleta fedha shilingi bilioni 4.5 kwa ajili ya kuwalipa fidia wananchi waliochukuliwa maeneo yao kwa ajili ya shughuli mbalimbali. Jumla ya wananchi 469 wanatarajia kulipwa kuanzia sasa, fedha tumezipokea tayari”. Akiongelea changamoto ya ‘double allocation’, alisema kuwa Rais alielekeza wananchi hao wa...