Kata ya Zuzu yajivunia mafanikio ya utekelezaji miradi ya maendeleo
Na. Valeria Adam, DODOMA SERIKALI yapongezwa kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayolenga kuboresha maisha ya wananchi wa Kata ya Zuzu ikiwa na matokeo chanya. Diwani wa Kata ya Zuzu, Awadh Abdallah Pongezi hizo zilitolewa na Diwani wa Kata ya Zuzu, Awadh Abdallah nje ya ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Diwani Abdallah alisema kuwa miradi ya ujenzi wa madarasa mapya, visima vya maji na barabara za lami inakwenda sambamba na malengo ya serikali ya kuhakikisha huduma bora kwa wananchi. Miradi hiyo imeanza kutoa matokeo chanya na wananchi wanaendelea kunufaika nayo. "Kwanza tunatekeleza mradi mkubwa wa Kituo cha Afya Zuzu kitakachogharimu shilingi milioni 550 na mpaka sasa takribani shilingi millioni 320 tumeshazipokea na ujenzi unaendelea. Tumejenga madarasa nane, matundu 16 ya vyoo na ofisi za walimu kwa ajili ya kidato cha tano na sita ambao tunatarajia mwaka unaofuatia tutaanza kuwa na wanafunzi wa kidato cha tano na sita. "Lakini pia tunaj...