Zabibu Hoteli Dodoma yajikita matumizi ya Nishati safi
Na. Mussa Richard, TAMBUKARELI Kampeni ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuhakikisha taasisi na sehemu zenye mkusanyiko wa watu zaidi ya 100 kutumia nishati safi ya kupikia, imepokelewa na kufanyiwa kazi ipasavyo na uongozi wa Zabibu Hoteli, iliyopo Kata ya Tambukareli jijini Dodoma. Hayo yamebainishwa na Meneja Mkuu wa Zabibu Hoteli, Mathew Gabriel, wakati akizungumza na vyombo vya Habari baada ya kutembelea hoteli hiyo ili kujionea matumizi ya nishati safi katika hoteli hiyo. āZabibu Hoteli ni miongoni mwa taasisi ambayo imejizatiti kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikia kwenye kila nyanja inayohusu mapishi. Nishati safi ya kupikia ni nzuri na ina faida nyingi kulinganisha na nishati zingine zinazochangia kwenye uchafuzi wa mazingira. Kwahiyo, niziombe sekta zote na watu binafsi wajikite katika matumizi ya nishati safi za kupikia kwasababu ni rahisi na salamaā alisema Gabriel. Nae, Focus Mwenda, Mpishi Mkuu wa Zabibu Hoteli, alimshukur...