Wazazi Chamwino washauriwa kutenga muda kuzungumza na watoto

Na. Dennis Gondwe, CHAMWINO WAZAZI na walezi katika Wilaya ya Dodoma wameshauriwa kutenga muda wa kukaa na kuongea na watoto wao ili waweze kubaini changamoto zinazowakabili ikiwemo kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia. Cpl. Edith Siwango kutoka Dawati la Jinsia na Watoto wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Dodoma alipokuwa akiongea na wanafunzi, walimu na wadau wa Lishe katika Shule ya Msingi Chamwino Ushauri huo ulitolewa na Cpl. Edith Siwango kutoka Dawati la Jinsia na Watoto wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Dodoma alipokuwa akiongea na wanafunzi, walimu na wadau wa masuala ya Lishe katika Shule ya Msingi Chamwino iliyopo Kata ya Chamwino Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Cpl. Siwango alisema “tupo hapa kwa ajili ya kuwalinda watoto wetu. Wazazi na walezi mlio hapa nawaomba mtenge muda wa kuzungumza na watoto wenu. Mazungumzo hayo yatawasaidia kuwaelewa watoto wenu. Watoto wamekuwa wakipitia changamoto mbalimbali zinazohusisha ukatili wa kijinsia na kushindwa kuwaeleza wazazi na ...