Posts

Showing posts from January 29, 2025

Matukio katika Picha wakati wa kukabidhi Taarifa ya ubainishaji wa watoto wenye mahitaji maalumu kwa mwaka 2025 Jiji la Dodoma

Image
 

Wataalam wa Mawasiliano na Maendeleo ya Jamii washiriki kubainisha watoto wenye mahitaji maalum

Image
Na. Aisha Ibrahim, DODOMA Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Fungo, aliwataka watumishi wa Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi, kuongeza wigo kwa kutumia wataalam wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Maendeleo ya Jamii ili kuhakikisha wanasambaza taarifa za uhamasishaji na kubainisha watoto wenye mahitaji maalumu katika jamii. Fungo aliyasema hayo ofisini kwake alipopokea taarifa ya ubainishaji wa watoto wenye mahitaji maalumu kwa mwaka 2025 kutoka Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi Jiji la Dodoma baada ya kukamilika zoezi la utambuzi na ubainishaji wa watoto wenye mahitaji maalum kwa jili ya kuandikishwa elimu ya awali na darasa la kwanza zoezi lililoanza 07 hadi 22 Januari, 2025. Akitoa pongezi kwa kazi nzuri ya ubainishaji wa watoto wenye mahitaji maalumu, Kaimu Mkurugenzi, alisema kuwa serikali inafanya juhudi kubwa kuhakikisha watoto hao wanapata haki stahiki na huduma za msingi ili kujiona wako sawa na binadamu wengine. “Mpaka serikali inafan...