Posts

Showing posts from June 12, 2026

Waziri Kikwete kufungua Wiki ya Kitaifa ya Utumishi wa Umma 2026

Image
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete Jumatano tarehe 17/06/2026 anatarajiwa kufungua Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2026 kwenye Viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma. Kaulimbiu ya Mwaka 2026 ni “ Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi kwa Maendeleo Endelevu ”

Kigamboni Vijana Unity wakabidhiwa Bajaji 5, Mkopo usio ya riba wa Jiji la Dodoma

Image
Na. Mwandishi wetu, DODOMA Kikundi cha Kigamboni Vijana Unity kutoka Mtaa wa Kigamboni, Kata ya Kikuyu Kaskazini kimekabidhiwa Bajaji tano kupitia mkopo usio na riba wa asilimia 10 unaotolewa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma kupitia Benki ya NMB ili kukiwezesha kikundi kujiajiri na kujikwamua kiuchumi. Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano hayo yaliyofanyika katika viunga vya Manispaa ya zamani jijini hapa, Kaimu Meneja wa Kanda ya Kati wa NMB, Amos Mubusi alisema kuwa benki hiyo inaendelea kushirikiana na serikali katika kuwawezesha vijana na makundi maalum ili kukuza biashara na kuongeza ushiriki wao katika uchumi. Mubusi alisema kuwa Benki ya NMB imetoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni tatu kwa vikundi 304 nchini, wakati Halmashauri ya Jiji la Dodoma, vikundi 19 vikipatiwa mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 228. Aidha, aliwataka wanachama wa Kigamboni Vijana Unity kutumia fursa hiyo kwa uwazi, nidhamu na uaminifu ili kuhakikisha mradi huo unaleta ...

Bodaboda Mtaa wa Kigamboni wanufaika na Kliniki ya kutatua kero

Image
Na. Mwandishi wetu, KIKUYU KASKAZINI MTAA wa Kigamboni umewatembelea maafisa usafirishaji kusikiliza changamoto zao na kuwaelezea fursa ya mikopo isiyo na riba ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa makundi ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu ili waweze kunufaika nayo. Akizungumza na maafisa usafirishaji wa Mtaa wa Kigamboni Kata ya Kikuyu Kaskazini, Afisa Mtendaji Mtaa wa Kigamboni, Farijala Kunga alisema kuwa serikali ina wajibu wa kuwatembelea na kuwasikiliza wananchi wake. “Leo Serikali ya Mtaa wa Kigamboni imewatembelea maafisa usafirishaji (waendesha bodaboda) katika Mtaa wa Kigamboni kusikiliza kero zao na kuzipatia ufumbuzi. Huu ni utekelezaji wa maelekezo ya serikali wa kuyafikia makundi mbalimbali kuyasikiliza na kutatua kero zao. Aidha, tumewaelezea fursa za mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri ya jiji la Dodoma kwa makundi ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu. Tumewapa elimu kuhusu manufaa ya kiuchumi ya mikopo hiyo ukiwa ...

Ujenzi wa madarasa 3 S/M Mazengo kukamilika Julai, 2026

Image
Na. Mwandishi wetu, KIKUYU KASKAZINI   Uongozi wa Mtaa wa Kigamboni, Kata ya Kikuyu Kaskazini umepongeza kasi ya ujenzi madarasa matatu katika Shule ya Msingi Mazengo kwa gharama ya shilingi 71,373,640 kwa lengo la kuboresha mazingira ya wanafunzi kujifunzia na kuelekeza mradi huo kukamilika kwa wakati.   Pongezi hizo zilitolewa na Afisa Mtendaji Kata ya Kigamboni, Farijala Kunga alipoongoza wajumbe wa Serikali ya Mtaa wa Kigamboni na maafisa ugani wa Kata ya Kikuyu Kaskazini kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa matatu katika Shule ya Msingi Mazengo. Alisema kuwa wameridhika na kasi ya ujenzi wa madarasa hayo ambayo yanatarajiwa kukamilika Mwezi Julai, 2026 kabla ya shule kufunguliwa. “Ni matumaini yangu kuwa ujenzi huu utakamilika kwa muda ulipangwa ili wanafunzi watakapofungua shule waweze kuyatumia. Madarasa haya ni utekelezaji wa ahadi ya Rais, kuleta tabasamu kwa wananchi, hapa ni wanafunzi na walimu watakaotabasamu” alisema Kunga. ...