Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Majengo Dodoma watarajia makubwa Mradi wa TACTIC
Na. Halima Majidi, DODOMA Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Majengo Jiji la Dodoma, wameishukuru serikali kwa kuona umuhimu wa kukarabati miundombinu ya Soko hilo na kuomba kuharakishwa uboreshaji wa soko ili waweze kuendelea na majukumu yao, kwa sababu soko hilo ndio soko mama la chakula. Akizungumza katika hafla ya Utiaji Saini Mikataba ya Ujenzi wa Miradi ya TACTIC uliofanyika katika Bustani ya Chinangali Park, Mfanyabiashara wa Soko Kuu la Majengo, Rhoda Boyi, alipongeza juhudi za Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kuwashirikisha katika hatua zote za mradi "Tunatarajia kuwa sauti zetu zitasikilizwa na kuzingatiwa ili kuhakikisha kuwa maboresho haya yanakidhi mahitaji yetu na kuboresha mazingira ya biashara" alisema Boyi. Kwa upande wake Mohammedi, alifafanua changamoto watakazokumbana nazo katika kipindi chote cha ukarabati wa jengo hilo, ni pamoja na; kupoteza wateja, kuharibika kwa bidhaa kutokana na kuhamishw...