Posts

Showing posts from 2026

Matukio katika picha hafla ya Uzinduzi wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Jiji la Dodoma

Image
 

Jukwaa la mifumo ya chakula lazinduliwa Dodoma

Image
Na. Rahma Magona, DODOMA   Jukwaa la Mifumo ya Chakula Halmashauri ya Jiji la Dodoma limezinduliwa leo katika Hoteli ya Mesuma jijini Dodoma, likiwa na lengo la kuimarisha uratibu na ushirikiano wa wadau katika kuhakikisha upatikanaji wa chakula bora na salama kwa wananchi.   Akizungumza katika uzinduzi huo, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Alimwoni Chaula, alisema kuwa jukwaa hilo litakuwa chombo cha uratibu kitakachowaunganisha wadau mbalimbali kwa ajili ya kubadilishana maarifa, uzoefu na rasilimali, pamoja na kutafuta suluhisho endelevu za changamoto zinazoweza kujitokeza katika mfumo wa chakula.   Alisema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma inaendelea kukua kwa kasi, hali inayoambatana na ongezeko la mahitaji ya chakula bora na salama, huku mfumo wa chakula ukitegemea uzalishaji kutoka katika mikoa mbalimbali nchini, ikiwemo Mbeya, Iringa na Morogoro.   Chaula alisisitiza kuwa changamoto katika mfumo wa chakula inahusisha mnyororo mzima...

Meya Chaula azindua Jukwaa la Mfumo wa Chakula Jiji la Dodoma

Image
Na. Mwandishi wetu, DODOMA   Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Alimwoni Chaula, amezindua rasmi Jukwaa la Wadau wa Mfumo wa Chakula katika Jiji la Dodoma kupitia Mradi wa ‘Growing Together’ unaotekelezwa na Taasisi ya Rikolto, kwa lengo la kuwakutanisha wadau mbalimbali na kujadili namna ya kuhakikisha upatikanaji wa chakula salama na chenye lishe katika Jiji la Dodoma.   Uzinduzi huo uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Mesuma, umewakutanisha wadau mbalimbali wa mfumo wa chakula, wakiwemo wakulima, wafanyabiashara, wawakilishi wa makampuni mbalimbali, taasisi na wadau wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, kwa ajili ya kujadili kwa pamoja fursa na changamoto zinazohusu uzalishaji, upatikanaji na uhifadhi wa chakula.   Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Meya Chaula alisema kuwa masuala ya mfumo wa chakula hayawezi kutekelezwa na mtu mmoja, bali yanahitaji ushirikiano kati ya serikali, sekta binafsi na wadau wengine, hususan kutokana na kasi ya ukuaji wa Jiji la Dodo...

Wakazi Mtaa wa Mazengo wapatiwa elimu ya Lishe

Image
Na. Ramadhani Mohammed, ZUZU Wakazi wa Mtaa wa Mazengo, Kata ya Zuzu jijini Dodoma, wamepatiwa elimu kuhusu umuhimu wa lishe bora kwa watoto, ikiwa ni sehemu ya kuongeza uelewa wa jamii kuhusu ulaji wa vyakula vyenye virutubishi muhimu kwa ukuaji na maendeleo ya watoto. Akizungumza baada ya kupata elimu hiyo, mkazi wa Mtaa wa Mazengo, Dorice Robert Mwibala alisema kuwa elimu hiyo imewasaidia kufahamu mambo mbalimbali ambayo awali hawakuwa wakiyajua kuhusu lishe ya watoto, huku akieleza kuwa itakuwa na manufaa kwa watoto na wajukuu wao. Alisema kuwa elimu hiyo imewafurahisha kwa kuwa imewapa uelewa muhimu kuhusu namna ya kuzingatia lishe bora kwa watoto, jambo analoona linaweza kusaidia kuboresha afya na maendeleo yao. Kwa upande wake, mkazi wa Dodoma, Ibrahimu Mgeni alisema kuwa elimu hiyo atawafikishia watu wake wa karibu ili nao waweze kufahamu umuhimu wa lishe bora, huku akiomba elimu kama hiyo iendelee kutolewa mara kwa mara katika jamii. Mgeni alisema kuwa hakuna jambo bora ...

Afisa Tabibu Zahanati ya Zuzu atoa elimu ya Lishe kwa vitendo

Image
Na. Ramadhani Mohammed, ZUZU Afisa Tabibu wa Zahanati ya Zuzu jijini Dodoma ametoa elimu ya lishe kwa wazazi na walezi kwa njia ya vitendo, akisisitiza umuhimu wa kuhakikisha watoto wanapata chakula bora na chenye virutubisho muhimu kwa ukuaji na afya zao. Akitoa elimu hiyo, Afisa Tabibu huyo aliwaonesha wazazi na walezi namna ya kuchagua na kuchanganya vyakula mbalimbali vinavyopatikana katika mazingira yao ili kupata mlo kamili unaokidhi mahitaji ya mtoto. Alisema kuwa lishe bora inaanzia katika familia, hivyo wazazi na walezi wanapaswa kuwa na uelewa sahihi kuhusu aina ya vyakula, namna ya kuviandaa pamoja na kiasi kinachofaa kwa watoto kulingana na mahitaji yao. Aidha, alisisitiza umuhimu wa kuzingatia usafi wakati wa kuandaa, kupika na kuhifadhi chakula, akieleza kuwa lishe bora ikiambatana na usafi husaidia kulinda afya ya mtoto na kupunguza hatari ya magonjwa. Alisema kuwa elimu hiyo imetolewa kwa vitendo ili kuwapa wazazi uelewa unaoweza kutumika moja kwa moja katika mais...

Siku ya Afya na Lishe Mtaa wa Bochela yawa fursa ya chanjo na elimu kwa jamii

Image
Na. Mwandishi wetu , NKUHUNGU Wananchi wa Mtaa wa Bochela, Kata ya Nkuhungu, jijini Dodoma, wameungana kuadhimisha Siku ya Afya na Lishe, ambapo wamepatiwa elimu ya lishe pamoja na huduma za chanjo kwa watoto wadogo. Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Muuguzi kutoka Jiji la Dodoma anayehudumu katika Kituo cha Afya Nkuhungu, Getrude Modest , alisema kuwa zoezi hilo ni sehemu ya kuwafikishia wananchi huduma za afya, hususan chanjo kwa watoto wenye umri wa miezi tisa na mwaka mmoja. Alisema kuwa chanjo hizo zinatolewa bila malipo, huku akiwapongeza wazazi na walezi kwa kuitikia kwa wingi na kuhakikisha watoto wao wanapata huduma hizo kwa wakati. Kwa upande wake, mwananchi wa Mtaa wa Bochela, Rehema Hafidhi , alisema kuwa zoezi hilo ni muhimu kwa jamii kwa kuwa linawawezesha wazazi kupata elimu ya afya na lishe pamoja na kupata huduma muhimu karibu na maeneo yao ya makazi. Aliomba viongozi na wataalamu wa afya kuendelea kuandaa matukio kama hayo mara kwa mara ili wananchi wengi zaidi ...

Mtaa wa Bochela wapewa elimu kupinga ukatili wa kijinsia

Image
Na. Mwandishi wetu, NKUHUNGU Wananchi wa Mtaa wa Bochela, Kata ya Nkuhungu, jijini Dodoma, walipatiwa elimu kuhusu ukatili wa kijinsia, aina zake, madhara pamoja na umuhimu wa kutoa taarifa kuhusu vitendo hivyo katik maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe ya Mtaa (SALiKI). Akizungumza wakati wa kutoa elimu hiyo, Inspekta Amina Shabani kutoka Polisi Kata ya Nkuhungu, alieleza kuwa ukatili wa kijinsia unahusisha matendo mbalimbali yanayosababisha mtu mateso au madhara kwa njia ya kimwili, kingono, kiuchumi au kihisia. Alifafanua kuwa miongoni mwa aina za ukatili wa kijinsia zilizotolewa elimu zilikuwa ukatili wa kimwili, ukatili wa kingono ikiwemo kulawitiwa, ukatili wa kiuchumi pamoja na ukatili wa kihisia. Aliwahimiza wananchi kuwa na uelewa kuhusu vitendo vya ukatili wa kijinsia na kutokaa kimya wanapobaini matukio hayo, badala yake wanatakiwa kutoa taarifa kwa vyombo husika ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa. Aidha, alisisitiza umuhimu wa jamii kushirikiana katika kuzuia vitend...

Picha za Matukio mbalimbali katika Uchaguzi na Uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Wilaya ya Dodoma

Image
 

Wananchi wapewa elimu ya Afya na Lishe bora Nkuhungu

Image
Na. Mwandishi wetu, DODOMA   Wananchi wa Mtaa wa Bochela, Kata ya Nkuhungu, jijini Dodoma, walipatiwa elimu kuhusu afya na lishe bora, hususan namna ya kuandaa chakula chenye virutubisho muhimu kwa watoto kuanzia umri wa miezi sita hadi miaka mitano.   Elimu hiyo ilitolewa wakati wa Siku ya Afya na Lishe ya Mtaa (SALiKI) ambapo kina mama walielekezwa umuhimu wa kumpatia mtoto chakula chenye mchanganyiko wa makundi mbalimbali ya vyakula kwa ajili ya ukuaji na afya bora.   Akitoa elimu hiyo, Mtaalamu wa Lishe kutoka Kituo cha Afya Nkuhungu, Getruda Modesti aliwaelekeza wazazi kuhakikisha watoto kuanzia miezi sita wanapatiwa vyakula vyenye virutubisho kutoka katika makundi muhimu ya vyakula, huku wakiendelea kunyonya hadi kufikia umri wa miaka miwili.   Makundi hayo yalihusisha mboga za majani, matunda yenye vitamini na madini, jamii ya mikunde, vyakula vya wanga vinavyoupa mwili nguvu, pamoja na vyakula vya kujenga mwili vyenye protini kutoka katika vyanz...

Maadhimisho ya SALIKI Kata ya Nkuhungu

Image
 

Dodoma kuanza awamu ya pili ya Kampeni ya Chanjo ya Polio tarehe 29 Septemba, 2026

Image
Na. Mwandishi wetu, DODOMA   Wazazi na walezi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma wametakiwa kuhakikisha watoto wanapata chanjo ya Polio katika awamu ya pili ya kampeni hiyo, inayotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 29 Septemba hadi tarehe 2 Oktoba, 2026.   Akizungumza katika kipindi cha Amka Tofauti kinachorushwa na Kituo cha Redio A FM, Afisa Tabibu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Ngoyeji Nkinga, alisema kuwa ushiriki wa wazazi na walezi ni muhimu katika kuhakikisha watoto wote wanaolengwa wanapata chanjo hiyo.   “Wazazi na walezi wahakikishe watoto walio chini ya miaka 10 wanapata chanjo ya Polio kwasababu chanjo hii ni salama na muhimu kwa watoto ili kuwalinda dhidi ya ugonjwa polio,” alisema Dkt. Nkinga.   Alisema kuwa chanjo ya Polio ina umuhimu mkubwa katika kuzuia madhara yanayoweza kusababishwa na ugonjwa huo, hivyo jamii inapaswa kuchukua hatua kuhakikisha watoto wanapatiwa chanjo kwa wakati.   Aidha, aliwataka wananchi kutoa us...

DC Shekimweri asisitiza urasimishaji biashara za wanawake

Image
Na. Paulo Paulo, VIWANDANI ​ Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri ametoa rai kwa wanawake wajasiriamali kutumia vema fursa ya uwepo wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi ili kukuza biashara zao na kuchangia katika maendeleo ya uchumi wa taifa.   ​ Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Wilaya ya Dodoma, aliwapongeza viongozi wapya waliochaguliwa na kuwataka kutekeleza majukumu yao kwa tija, uadilifu na ushirikiano mkubwa na serikali pamoja na mamlaka husika.   ​ Sambamba na hilo aliwataka wajasiriamali kurasimisha biashara zao ili kuongeza fursa za kutambulika, kupata masoko mapya, na kufaidika na fursa za uwekezaji na mikopo pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuendelea kutoa elimu, ushauri, na kujenga mahusiano mazuri na wafanyabiashara wadogo badala ya kulenga ukusanyaji wa kodi pekee.   ​ Aliwahimiza wanawake kutumia teknolojia ya kidijitali na mifumo ya kisasa katika kutafuta masoko na kusimamia fedha za ...

Eneo lililoathiriwa na moto Soko la Machinga kurejea ndani ya siku 10

Image
Na. Mwandishi wetu, DODOMA Soko la wazi la Machinga lililoathiriwa na moto mkubwa uliotokea tarehe 20 Septemba, 2026 linatarajiwa kurejea katika hali ya kawaida ndani ya siku 10, huku Halmashauri ya Jiji la Dodoma likianza kuchukua hatua za kurekebisha maeneo yaliyoathirika na kuboresha mpangilio wa biashara. Hayo yalisemwa na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Alimwoni Chaula baada ya kutembelea soko hilo kwa lengo la kukagua madhara yaliyosababishwa na moto huo na kutoa pole kwa wafanyabiashara wa soko hilo. “Leo tumekuja kujionea madhara waliyopata wafanyabiashara wetu wa machinga ambapo juzi ulitokea moto mkubwa ambao uliathiri vibanda mbalimbali vya wafanyabiashara wa Dodoma. Pia nitoe pongezi kwa uongozi wa mkoa na wilaya, Jeshi la Polisi pamoja na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kusaidia kuzuia moto huo kusababisha madhara makubwa zaidi,” alisema Chaula. Alisema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma inatekeleza maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kuhakikisha waf...