Posts

Showing posts from August 10, 2025

RC Dodoma apongeza wafugaji kwa ushiriki wa Paredi ya Mifugo

Image
Na. Veronica John, DODOMA Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule awapongeza wafugaji kwa kujitokeza kwa wingi katika shindano la Paredi ya Mifugo Kitaifa 2025 ambalo hufanyika kila mwaka kuanzia tarehe 1-8 Agosti. Akizungumza na wafugaji, Senyamule alisema kuwa ameshuhudia mabadiliko na maboresho makubwa katika shughuli za mifugo ambapo hapo awali ilifanyika kikanda na sasa yameenda kimataifa. Alisema kuwa mashindano hayo kufanyika sehemu nyingi duniani yakiwa na lengo la kutambua mchango na juhudi za wafugaji katika kuchangia maendeleo ya taifa na ya mtu mmoja mmoja. “Maonesho haya huongeza ari kwa wananchi katika kuinua hadhi ya uzalishaji na tija kwa kutumia teknolojia mpya zilizoboreshwa katika shughuli za ufugaji ili kukidhi mahitaji ya soko. Na nimearifiwa kuwa maonesho na mashindano haya yaliasisiwa na Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2010 katika siku ya kilele cha sherehe za maonesho ya Nanenane Dodoma” a...

Elimu ya utunzaji zao la Zabibu yawafikia wananchi Jiji la Dodoma

Image
Na. Veronica, NANENANE DODOMA   Afisa Kilimo Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Emanuel Mayyo ametoa elimu juu ya utunzaji wa kilimo cha zabibu kuanzia upandaji hadi uvunaji ili kiwe na tija kwa wakulima. Hayo aliyasema katika viwanja vya maonesho ya Nanenane wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea vipando bustani vya Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Alisema kuwa kuna umuhimu wa kulima zao la zabibu kwasababu ni zao lenye faida katika sekta ya biashara na kuwakwamua kiuchumi wananchi wa Jiji la Dodoma. “Zao la zabibu ni zao mama hapa Dodoma na ni zao ambalo linafaida kubwa kwa wakulima. Hivyo, kuna haja ya wale wakulima ambao wanahitaji kulima zao hili kujifunza na kutambua hatua zote za zao hili kuanzia upandaji hadi uvunaji ili kupata zao bora,” alisema Mayyo. Pia aliongeza kusema kuwa kuna mpango wa kuweka mkataba na baadhi ya makampuni ili wananchi wa Jiji la Dodoma waweze kupata soko la zao hilo. “Vilevile, tuna mpango madhubuti kwa wale wakulima ...

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa Pamoja na viongozi mbalimbali kabla ya kuaga mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Job Yustino Ndugai katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma tarehe 10 Agosti, 2025

Image
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha Maombolezo mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma kwa ajili ya kuongoza waombolezaji kuaga mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Job Yustino Ndugai tarehe 10 Agosti, 2025

Image
 

Zao la Zukini na faida lukuki

Image
Na. Rehema Kiyumbi, DODOMA Afisa Kilimo Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Nkunde Kimweri amesema kuwa zao la zukini ni zao lenye vitamini ambalo hutumika kama kiungo cha mboga ili kuleta ladha na kiafya hutumika kupunguza shinikizo la damu. Alisema kuwa zao la zukini ni jepesi kupanda na lina matokeo mazuri. ’’Tulitumia mbolea na dawa kutoka Kampuni ya Fomi kuzia na baadae tukatumia Fomi nenepesha ilipoanza kutoa maua. Pia tulitumia dawa ya 40-44 kutoka Kampuni ya Jumbo kudhibiti wadudu na kuhakikisha usalama na ubora wa zao letu, lakini pia tunamshukuru Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kwa kutuletea vitu muhimu katika kukuza mazao yetu na hatujapata changamoto yoyote hadi hapa tulipofikia,” alisema Kimweri. Alimalizia kwa kuwashauri vijana walio jumbani wakati wakisubiri ajira wajikite katika kilimo ili kujipatia kipato. ’’Tunawashauri vijana wachukue mikopo inayotolewa na halmashauri ili wajikite katika kilimo na kujikwamua kiuchumi katika maisha yao na kama tunavyofahamu kilimo kinamto...

Zao la Nyanyachungu na Bilinganya linafaida kwa jamii

Image
Na. Rehema Kiyumbi, DODOMA Afisa Kilimo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Nkunde Kimweri    ametoa elimu kuhusiana na zao la nyanyachungu na bilinganya kwa kuanisha uandaaji, matumizi sahihi ya mbolea na matumizi ya dawa ya kudhibiti wadudu wanaoathiri zao hilo kwa lengo la kukuza uchumi kwa wafanyabiashara na matumizi ya nyumbani. Akizungumza na mwanahabari katika vipando vya Halmashauri ya Jiji la Dodoma alisema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa mazao hayo hasa kwa wafanyabiashara. “Tulianza kwa kuandaa shamba la zao la bilinganya aina ya ‘black beauty’ na nyanyachungu aina ya ‘tengeru white’ kwa umbali wa sentimita 60 kwa sentimita 60 ili kuwezesha mmea kuweza kujitanua na kukua kwa uhuru na tulitumia mbolea kutoka Kampuni ya Yara ambapo ni Yara oteshi, na Yara kuzia wakati wa kukuzia mmea wetu na tukatumia dawa viwatilifu kwa kuulia wadudu wanaoshambulia kwa kasi sana zao hili,” alisema Kimweri.   Naye, msimamizi wa bustani Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Milton Edwa...