KAMATI YA SIASA MKOA WA DODOMA YAPONGEZA USIMAMIZI UJENZI SHULE YA MIYUJI B

Na. Dennis Gondwe, MIYUJI KAMATI ya Siasa ya Mkoa wa Dodoma imepongeza usimamizi mzuri wa shule mpya inayojengwa ya Miyuji B iliyopo Kata ya Miyuji jijini Dodoma na kusema kuwa shule hiyo itawapunguzia hadha ya kutembea umbali mrefu wanafunzi. Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma, Pili Mbaga akisisitiza jambo Pongezi hizo zilitolewa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma, Pili Mbaga alipoongoza Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Dodoma kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule mpya ya Miyuji B inayojengwa Kata ya Miyuji. Mbaga alisema “nimpongeze mkuu wa shule jirani ya Miyuji anayesimamia ujenzi wa shule hii kwa kazi nzuru na usimamizi mzuri. Hakika majengo ni mazuri na yanapendeza. Aidha, niwapongeze na wahandisi kwa kusimamia vizuri shule hii. Maeneo mengine wahandisi hawasimamii miradi ya ujenzi jambo linalopelekea miradi mingi kujengwa chini ya kiwango kwa kukosa usimamizi”. Vilevile, kiongozi huyo wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Dodoma alielezea kufurahishwa kwake kwa taa...