ILEMELA MANISPAA YAVUTIWA UWEKEZAJI MIRADI YA KIMKAKATI DODOMA
Na. Tutindaga Nkwindi, DODOMA MADIWANI wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela wamevutiwa na uwekezaji na utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma na kulitaja kuwa ni jiji darasa. Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Kuruthum Abdallah baada ya kutembelea miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Alisema kuwa wamevutiwa na kiwango cha uwekezaji pamoja na usimamizi madhubuti miradi hiyo na kubainisha kuwa Ilemela inakwenda kutumia uzoefu huo kama darasa. Tunaipongeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kumiliki na kuendesha miradi mikubwa na yenye tija kama hii. Sisi pia tuna miradi inayofanana na hii. Hivyo, ziara hii imetupa nafasi ya kujifunza mambo mengi ambayo tunaenda kuyafanyia kazi Ilemela ili tuweze kuboresha huduma na kuongeza mapato yetu ya ndani kupitia miradi ya kimkakati ” alisema Abdallah. Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispa...