Dodoma Jiji FC, yatua Dar kibabe kumenyana na Mnyama
Na. Mussa Richard, Klabu ya Soka ya Dodoma Jiji FC, itashuka dimbani hapo kesho kumenyana na klabu ya Soka ya Simba SC, katika mchezo wa ligi kuu ya NBC Tanzania bara, mchezo utakaopigwa katika dimba la KMC Complex Mwenge, Dar es salaam majira ya saa 10 kamili jioni. Akizungumzia maandalizi ya timu, Kocha mkuu wa Dodoma Jiji FC, Mecky Mexime wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa Simba SC, alisema ātunamshukuru Mungu tumefika Dar es Salaam salama, jana tumefanya mazoezi mepesi ya kuiweka miili sawa, tunajua mchezo utakuwa ni mgumu kwa pande zote, ukizingatia kwasasa ligi inaelekea ukingoni. Alama tatu kwa kila mchezo ni muhimu ili tuweze kifikia malengo yetu ya kumaliza ligi tukiwa nafasi za juu kwenye msimamo, maandalizi yote ya kucheza na Simba SC, tumeyafanya tukiwa Dodoma. Hapa tumekuja kukifanyia kazi kile tulichojifunza kwenye uwanja wa mazoeziāā. Nae Abdi Banda, mchezaji wa Klabu ya Soka ya Dodoma Jiji FC, akawaita mashabiki wa Dodoma Jiji FC, waliopo Da...