Posts

Showing posts from June 19, 2026

Ofisi ya Waziri Mkuu yathibitisha nyenzo muhimu za kuimarisha usimamizi wa maafa nchini

Image
Na. Mwandishi wetu, DODOMA   SERIKALI imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha mifumo ya usimamizi wa maafa nchini ili kuongeza uwezo wa kuzuia, kujiandaa, kukabiliana na kurejesha hali baada ya maafa, kufuatia kuongezeka kwa matukio yanayochochewa na mabadiliko ya tabianchi pamoja na vihatarishi vingine vya asili na kijamii.   Hayo yalielezwa jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Brigedia Jenerali Hosea Ndagala, wakati akifungua Kikao cha Jukwaa la Taifa la Wadau wa Usimamizi wa Maafa kilicholenga kupitia na kuthibitisha Mwongozo wa Urejeshaji Hali Baada ya Maafa, Mwongozo wa Uendeshaji na Uratibu wa Uhawilishaji Fedha kwa Walioathirika wa Maafa, pamoja na Mfumo wa Usimamizi wa Taarifa za Maafa (DMIS).   Brigedia Jenerali Ndagala alisema kuwa katika miaka ya hivi karibuni Tanzania imekumbwa na matukio mbalimbali ya maafa yakiwemo mafuriko, ukame, maporomoko ya ...

Waziri Kikwete Ahimiza Uwajibikaji na Ubunifu kwa Watumishi wa Umma

Image
Na. Bupe Mwaiseje - MAELEZO Watumishi wa umma nchini wamehimizwa kuzingatia uwajibikaji na ubunifu katika kutekeleza majukumu yao ili kuboresha huduma za Serikali zinazotolewa kwa wananchi. Akizungumza katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete wakati akifungua Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma, amesema kuwa Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi wa umma ili kuwawezesha kutoa huduma bora na zenye ufanisi.   Ambapo alitoa wito kwa watumishi wa umma kuiishi kauli mbiu ya mwaka 2026 inayosema “Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi kwa Huduma Endelevu” inayolenga kuwakumbusha watumishi hao wa umma kutambua nafasi yao katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma zinazostahili. “Niwaombe watumishi wa umma wote kuuishi ujumbe huu, kwani uwajibikaji ndio msingi wa uongozi na utumishi wa umma unaozingatia mahitaji ya wananchi,” amesisitiza Mhe. Kikwet...

Waziri Mkuu aagiza usimamizi mzuri wa mitambo ya uchimbaji Visima

Image
Awataka watendaji kuacha mazoea katika utekelezaji wa majukumu   Na. Mwandishi wetu, WAZIRI Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka watendaji wa Wizara ya Maji pamoja na Wakuu wa Mikoa wasimamie vizuri mitambo ya uchimbaji visima ili iweze kufanya kazi iliyokusudiwa. Alisema kuwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan alinunua mitambo ya uchimbaji wa visima hivyo watendaji wachukue hatua na waache kufanya kazi kwa mazoea. “Nielekeze wakuu wa mikoa yote pamoja na wizara, kusimamia ili mitambo ile iweze kufanya kazi iliyokusudiwa, ni kweli kuna baadhi ya maeneo ya tunaendelea endelea na ile tabia ya ‘business as usual’ sasa ili kufikia matokeo ya Dira 2050, ni lazima tufanye kazi ‘business unusual’ tuache kufanya kazi kwa kuchukulia vitu kimazoea mazoea", alielekeza Waziri Mkuu. Dkt. Mwigulu alitoa maelekezo hayo leo (Alhamisi Juni 18, 2026) Bungeni jijini Dodoma katika kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu wakati akijibu swali la Mbunge wa Kwimba, Cosmas Bullala. Mbunge huyo alitaka ku...