Posts

Showing posts from November 13, 2025

Chupa 41 za damu zakusanywa Nyerere Square, wananchi wahimizwa kuendelea kuchangia

Image
Na. Nancy Rogers, DODOMA Jumla ya chupa 41 za damu zilikusanywa kutoka kwa wachangiaji waliojitokeza kwa hiari katika siku ya kwanza ya Kliniki ya Upimaji Magonjwa y asiyoambukiza inayoendelea katika bustani ya mapumziko Nyerere Square jijin Dodoma . Uchangiaji huo wa damu umehimizwa kufanyika kila wakati kwa lengo la kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji damu kwa dharura hospitalini, huku wakazi wakihimizwa kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hilo muhimu la kuokoa maisha. Hayo yalielezwa na Mkuu wa Timu za Ukusanyaji Damu Kanda ya Kati kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Leah Kitundya ambae alisema kuwa lengo la kampeni hiyo ni kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa kuchangia damu mara kwa mara, kwasababu mahitaji ya damu katika hospitali yanaongezeka kila siku. “Tunaendelea kuhimiza jamii kuchangia damu kwa hiari, kwa kuwa damu ni uhai na inaweza kuokoa maisha ya mama wajawazito, wagonjwa wa upasuaji na wa ajali” alisema. Mmoja wa wachangiaji damu na Mkazi wa Miyuji, Rehema J...