Kituo cha Afya Ilazo mkombozi kwa wananchi
Na. Mwandishi wetu MRADI wa ujenzi wa Kituo cha Afya Ilazo utakapokamilika utahudumia wananchi 99,743 wa Kata ya Nzuguni na maeneo ya jirani ikiwa ni mkakati wa serikali ya awamu ya sita wa kusogeza huduma za afya karibu na wananchi. Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Andrew Method alipokuwa akisoma taarifa mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Ilazo kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2024. Dkt. Method alisema kuwa lengo la mradi huo ni kuboresha huduma za mama na mtoto na huduma za upasuaji ukitarajiwa kuhudumia zaidi ya wananchi 99,743 wa Kata ya Nzuguni, Ipagala na maeneo menginge watapata huduma bora za afya mradi huo utakapokamilika. Akiongelea mafanikio ya mradi huo, aliyataja kuwa ni kuwezesha kutoa huduma za upasuaji, kliniki ya mama na mtoto, huduma za kujifungua, wodi ya watoto wachanga , huduma za kuhifadhi miili. Mafanikio mengine ni “wodi hizi pia zimeunganishwa na mi...