Madiwani wadaiwa uthubutu kufanya maamuzi ya kimaendeleo
Na. Faraja Mbise, DODOMA Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera, wametakiwa kuwa na uthubutu katika kufanya maamuzi ya kimaendeleo ili kuwanufaisha wananchi wanaowasimamia. Hayo yalisemwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe, alipokuwa akiwakaribisha madiwani kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera, katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Mstahiki Meya, Prof. Davis Mwamfupe akifafanua jambo “Kikubwa katika mtakachokiona, sio utajiri wetu wa pesa ni uthubutu wa kufanya maamuzi, unaweza kuwa na pesa lakini hauna uthubutu wa kuzitumia, ukipewa shilingi milioni moja, utapata wasiwasi kuzitumia kwasababu zitaisha, hutakubali matumizi ya laki mbili au tatu. Lakini sisi hatuogopi, kama tuna mradi wa hoteli iliyopo hapa ambayo imegharimu shilingi Bilioni 12, hatuogopi mradi wa Soko la wazi la Machinga, ingawa serikali ilituchangia shilingi Bilioni tatu, na sisi tukaweka shilingi bilioni sita nyingine. Hatuogopi kwamb...