Mradi wa majaribio wa usimamizi taka kuanza Dodoma
Na. Asteria Frank, DODOMA Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira wanatekeleza mradi wa majaribio wa usimamizi wa taka za plastiki katika Jiji la Dodoma kwa lengo la kuhamasisha njia bunifu katika usimamizi wa taka za plastiki kupitia dhana ya uchumi rejeshi ili kupunguza taka za plastiki kwenye mazingira na kuboresha maisha na uchumi wa taifakwa ujumla. Baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya mradi huo uliopo katika Kata ya Chamwino, Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Aliy Mfinanga, alisema kuwa mradi wa majaribio utawanufaisha na kuwawezesha jamii na vikundi vya usafi kufanya shughuli za ukusanyaji na usafirishaji wa taka katika Kata ya Chamwino kwa nia ya kutia thamani kupitia dhana ya uchumi rejeshi ili kutunza Mazingira kutokana na plastiki. “Tumeshazoea kuona msisitizo mkubwa kuwa taka ni taka na kwamba haifai tena, lakini kupitia mradi huu wa majaribio tunataka kuonesha jamii kuwa tunaweza kuongeza...