Duka la Kuuza Viwanja kutoa huduma Jumamosi Tarehe 10 Januari, 2026
Na. Mwandishi Wetu, DODOMA Ofisi za Halmashauri ya Jiji la Dodoma zitakuwa wazi siku ya Jumamosi tarehe 10 Januari, 2026 kuanzia saa 2:30 hadi saa 9:30 alasiri kwa lengo la kuwahakikishia huduma bora hasa upatikanaji wa ‘control number’ za malipo ya viwanja ndani ya muda wa notisi ya halmashauri ya siku 21. Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikali Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dennis Gondwe alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu maelekezo ya Mkurugenzi wa Jiji hilo juu ya ofisi hizo kufunguliwa siku ya Jumamosi, tarehe 10 Januari, 2026. “Ndugu waandishi wa habari, napenda kuwatangazia kuwa katika kufanikisha utekelezaji wa Notisi ya siku 21 ya kulipa madeni ya viwanja kwa wananchi waliochukua viwanja eneo la Mtumba Zone II, III na Kikombo kuanzia tarehe 30 Desemba, 2025 inayokamilika tarehe 19 Januari, 2026. Hivyo, mkurugenzi ameagiza ofisi za halmashauri iliyokuwa manispaa ya zamani duka la kuuza viwanja ziwe wazi kuanzia saa 2:30 asubuhi hadi sa...