Posts

Showing posts from May 10, 2025

UMISSETA kuandaa vijana katika sekta ya Michezo Dodoma

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA MASHINDANO ya Umoja wa Michezo wa Shule ya Sekondari Tanzania (UMISSETA) ni takwa la kikanuni katika mitaala ya sekta ya elimu kwa lengo la kuwaandaa wanafunzi kuwa mahili katika sekta ya michezo Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Michezo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Peter Ititi alipokuwa akiongelea maandalizi ya michezo hiyo jijini Dodoma. UMISSETA ni michezo muhimu kwa wanafunzi na Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa ujumla. “Michezo imetajwa kwenye mitaala ya elimu kutokana na umuhimu wake. Michezo hiyo inalenga kuibua vipaji na kuviendelea kwa maslahi mapana ya taifa. Michezo pia ni ajira na tumekuwa tukishuhudia vijana wetu wakishiriki katika ligi mbalimbali” alisema Ititi. Alisema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Mwaka 2024 ilitoa wanafunzi 56 kati ya wanafunzi 120 waliochaguliwa kuunda timu ya UMISSETA ya Mkoa wa Dodoma iliyoshiriki kitaifa. “Mwaka huu matarajio yetu ni kuchukua makombe yote na tumejipanga kupele...

UMISSETA Jiji la Dodoma yaanza Dodoma Sec

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA MASHINDANO ya Umoja wa Michezo wa Shule ya Sekondari Tanzania (UMISSETA) ngazi ya kanda za Halmashauri ya Jiji la Dodoma yameanza katika viwanja vya Shule ya Sekondari Dodoma kwa lengo la uunda timu ya jiji hilo itakayoshiriki katika mashindano ngazi ya halmashauri ili kuunda timu ya Mkoa wa Dodoma. Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Michezo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Peter Ititi alipokuwa akiongelea maandalizi ya michezo hiyo jijini Dodoma. Ititi alisema kuwa halmashauri iliunda kanda sita zikiwa na shule tofauti tofauti za sekondari kwa lengo la kuzishindanisha. “Kila kanda ilitoa timu moja inayoshiriki michezo yote. Hivyo, baada ya mashindano haya itaundwa timu ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma itakayoshindana na timu za halmashauri nyingine ili kuunda timu ya Mkoa wa Dodoma” alisema Ititi. Michezo inayochezwa katika mashindano ya UMISSETA ni mpira wa miguu kwa wavulana na wasichana, mpira wa mikono wavulana na wasichana, mpira wa wavu wavulana n...

Kata ya Kizota yajivunia maendeleo makubwa ya miradi

Image
Na. Asteria Frank, DODOMA Diwani wa Kata ya Kizota, Jamal Ngallya afurahia mafanikio ya serikali kwa kipindi cha miaka minne ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Kituo cha Afya, Shule ya Msingi Mahungu na stendi ya mabasi katika kata yake. Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea kata hiyo kujionea miradi iliyotekelezwa na serikali katika Kata ya Kizota. Alisema kuwa katika kipindi cha miaka minne ya serikali ya awamu ya sita, kata hiyo imeshuhudia maendeleo makubwa. “Mimi leo naweza kuzungumza kuwa Kizota ya sasa hivi na ya miaka 10 nyuma ni vitu viwili tofauti, wakati mimi nazaliwa tulikuwa tunapata huduma za afya Makole na taasisi ya Magereza Isanga lakini leo Kizota tunatamba tumepata kituo cha afya kikubwa ambacho kinagharimu kiasi cha zaidi ya shilingi 500,000,000 ambapo kwa Dodoma sasa hivi kituo hicho kitashika nafasi ya tatu kwa ukubwa na hivi karibuni kitaenda kufunguliwa ili kitoe huduma mbalimbali kwa wananchi” alisema Ngallya. Ali...

Miaka minne ya Dkt. Samia, Kizota yanufaika mikopo ya asilimia 10

Image
Na. Coletha Charles, KIZOTA Wananchi wa Kata ya Kizota Halmashauri ya Jiji la Dodoma, waeleza kunufaika na mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri kwa makundi ya wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu, ikiwa ni hatua ya kuinua maisha yao kiuchumi na kuimarisha shughuli zao za ujasiriamali. Walieleza hisia zao mbele ya waandishi wa habari waliofanya ‘media tour’ kutembelea miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na serikali katika Kata ya Kizota kuanzia mwaka 2021 hadi 2025. Akizungumzia hali ya mikopo hiyo, Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Kizota, Theresia Ntui alisema kuwa tangu kuanza kwa utolewaji mikopo ya asilimia 10 katika serikali ya awamu ya sita, Kata ya Kizota imenufaika kwa jumla ya shilingi 410,000,000 zilizotolewa kwa vikundi mbalimbali vya kijamii. Alisema kuwa katika fedha hizo, vikundi 28 vya wanawake vilipokea shilingi 192,000,000 vikundi 16 vya vijana vilipewa 164,000,000 na vikundi vitano vya watu wenye ulemavu walipata shilingi 49,000,000. “Mikopo hii ni ...

Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

Image
Na. Coletha Charles, KIZOTA WANANCHI wa Kata ya Kizota Halmashauri ya Jiji la Dodoma, wanufaika na mradi wa ujenzi wa kituo cha afya kilichogharimu kiasi cha shilingi 500,000,000 kwa lengo la kusogeza huduma ya afya kwa wakazi wa kata hiyo. Viongozi na wananchi wa kata hiyo wamemshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kuhakikisha huduma ya afya inaboreka nchini kote hususan katika Kata ya Kizota. Aidha Diwani wa Kata ya Kizota, Jamal Ngallya alisema kuwa kukamilika kwa kituo hicho kutaboresha kwa kiwango kikubwa upatikanaji wa huduma za afya kwa wakazi wa Kizota na maeneo jirani. “Kituo chetu kimejengwa kwa gharama kubwa sana, jumla ya shilingi 500,000,000 zimeletwa na serikali kukamilisha mradi huo ili wananchi wapate huduma nzuri na bora. Majengo yaliyojengwa katika kituo hiki ni pamoja na jengo la wagonjwa wa nje, jengo la mionzi, jengo la huduma ya mama na mtoto, jengo la maabara, kichomea taka, na yataongezwa majengo mengine kama wodi za wagonjwa pamoja na...

Mavunde awanufaisha wakazi wa Kata ya Kizota

Image
Na. Asteria Frank, DODOMA Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Relini, Kata ya Kizota, Lizi Edward amshukuru Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde kwa kuwanufaisha wananchi kupitia miradi ya maendeleo ya elimu kwa kuanzisha ujenzi wa Shule ya Msingi Mbuyuni kwa lengo la kupunguza msongamano wa wanafunzi. Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na serikali katika Kata ya Kizota. “Kipekee nipende kumshukuru Mhe. Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde kwa kutuletea na kutusapoti kuanzisha ujenzi wa shule ya Mbuyuni ambapo kwa kushirikiana na nguvu za wananchi tumefanikiwa kujenga madarasa sita na ofisi mbili ambapo bado haijakamilika. Pia tunaishukuru serikali kwaajili ya kutupatia mradi wa kituo cha afya kwaajili ya kutoa huduma na kuboresha afya za wananchi” alisema Edward. Kwa upande wake Mwalimu wa shule ya Msingi Mahungu, Mwl. Donatus Gagula, alisema kuwa shule imeanza kujengwa mwezi Oktoba 2024, kupitia mradi ...