Timu ya Pete ya Combine yatubu kwa Timu ya Elimu Msingi
Na. Coletha Charles, DODOMA Timu ya Mpira wa Pete ya Elimu Msingi imeibuka na ushindi wa kishindo kwa kuifunga Timu ya Combine (Elimu Sekondari na Watendaji wa kata) kwa mabao 9-5 ambapo mchezo huo ulifanyika kwenye uwanja wa Jamhuri, ukiwa na ushindani mkubwa huku kila upande ukionesha mchezo wa hali ya juu. Mchezo ulianza kwa kasi huku Timu ya Elimu Msingi ikiongoza katika robo ya kwanza kwa mabao 4-1 wakitumia uzoefu wa wachezaji wao wakongwe. Hata hivyo, Combine walionesha nidhamu ya hali ya juu na kutumia mbinu bora za kiufundi, katika robo ya pili timu zote ziliongeza kasi ili kupata alama muhimu za ushindi huo wa kihistoria. Kocha wa timu ya Elimu Msingi, Emma Ernest, alisema kuwa, walishinda kwa sababu nyumba bila msingi hauwezi kujenga. Hivyo, waliweka msingi imara ndio maana waliweza kushinda kwa kishindo kwa kufanya mazoezi. “ Tulijiandaa vya kutosha kwa mchezo huu. Wachezaji wangu wameonyesha nidhamu, umoja, na uwezo wa kupambana hadi dakika ya mwisho. Ushindi huu ni ...