Wananchi watakiwa kuwa msitari wa mbele kupinga ukatili
Na. Coletha Charles, CHAMWINO Wakazi wa Kata ya Chamwino, Halmashauri ya Jiji la Dodoma walipewa elimu dhidi ya ukatili wa kijinsia na malezi bora ambayo imetolewa katika Ofisi ya Afisa Mtaa wa Mwaja kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kutambua yanayoendelea kwenye jamii. Akizungumza na wakazi wa eneo hilo, Mratibu wa Jinsia na Watoto, Fatuma Kitojo amewataka wazazi hao kuwa walezi bora kwa watoto wao na kutowatamkia maneno mabaya ambayo yanawakatili kisaikolojia ili wakubalike na jamii inayo wazunguka. Kitojo alisema kuwa ni muhimu kwa wazazi kuelewa kwamba maneno wanayosema yanaweza kuwa na athari kubwa kwa maendeleo ya watoto kihisia, kujitambua, na uhusiano mzuri na Watoto wengine. “Watoto wetu wanatupenda sana na wanapenda kuona sisi tunafanikiwa ni kweli tuna shughuli nyingi tunakimbizana na muda na maisha kwa sababu za hali za kiuchumi na mabadiliko ya sayansi na teknolojia. lakini tunajua kwa asili mwanamke ndiyo mlezi namba moja. Kwahiyo tunatakiwa tutenge mda wa ...